NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA TANO(45)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Farudume akakimbia haraka na kuwasha gari lake tayari kwenda na yeye mwenyewe kushuhudia tukio hilo la kipekee na la muhimu ambalo lilikuwa likikaribia kutimizwa na Tinonko, yaani kuwaonesha sehemu mali zilipo.
Farudume akiwa ni mtu pekee aliyewatonya watafiti hao wa Kizungu kuhusu habari za mali hizo katika msitu wa Congo na hatimaye kuwauzia Tinonko, alipaswa kupewa asilimia 50 ya kila mali itakayovunwa na wazungu hao; kwa maana hiyo basi lazima naye atakuwa tajiri wakutupwa.
Alipofika alikaribishwa haraka na kuingia ndani akafikia kutumbua macho kwenye skrini kubwa ambayo iliyoonesha kidoti chekundu ambacho kilikuwa kikitembea, kwa mujibu wa wazungu hao walisema kuwa huyo ni Tinonko. 
Wote walisubiri kidoti kile kisimame kwanza, maana kitakapotulia tu kwa muda wa takribani nusu saa na kuendelea, basi hapo ndipo walipokadiria kuwa ndiyo kwenye mali yenyewe, yaani mbirikimo watakuwa wamefika mwishoni mwa safari yao.
Hivyo wakatulia ili kusubiri kidoti hicho kitulie. Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa wakaona kidoti kimetulia kisha wakasubiri nusu saa na kugundua hakitembei tena. Hapo haraka wataalamu wakasoma latitudo na longitudo ilikujua lokesheni aliyopo Tinonko. 
Wakaanza kujipongeza kwa vinywaji huku haraka wakatumwa makomando kuvamia ile sehemu alipotuama Tinonko.
Muda huohuo Helikopta kama sita zilionekana kutua kwenye msitu wa Kongo, na tukio zima likaoneshwa wazi kupitia kamera za video zao. Makomando wakaonekana kutua katikati ya msitu wakiwa na kila aina ya silaha. Wakashuka kwa tahadhari na kuanza kutawanya majani na vichaka virefu wakisaka GPS ya sehemu ambayo ilionesha Tinonko alipokuwepo.
Kitu cha kushangaza ni kwamba, mitambo yao ya ‘GPS Tracker’ ilikuwa imeelekeza kwa Sokwe mtu aliyeonekana amelala tuli kwenye mti. Walipomfikia alionekana kukimbia akiwakwepa wawindaji wake walioonekana kupigwa na butwaa.

Kule makao makuu ya utafiti wakaanza kujiuliza imekuaje.
Ghafla bastola zikaelekezwa kwa Farudume aliyewekwa chini ya ulinzi. Mr. Duncan akaonekana kujaa hasira sana akasema; “It’s impossible Faru, you’ve double crossed me? (haiwezekani Faru, umenizunguka?)”
Farudume akawashangaa wazungu hao walioonekana kuchachamaa kwa sababu ambayo hakuijua hata kidogo. “Hii kazi ni yetu wote, kwanini niwazunguke, unanidissappoint, Mr. Duncan!” alisema Farudume akiwa ameketi kwenye kiti, huku wale wazungu wengine wakionekana kumsachi na kuchukua silaha zake zote.
“Mr. Henry bring them in!” (Mr Henry walete ndani) wakati huo mlango ukafunguliwa na kuonekana watu wakiingia taratibu ndani ya chumba kile cha mitambo walichokuwemo wakina Farudume na wenzake.
Kutahamaki walikuwa ni Uku-Uku na Eddy ambaye ni mdogo wake Farudume Yule mlemavu ambaye siku zote Farudume amekuwa akimlaumu Tinonko kwa yaliyomkuta, kama kawaida akiburuzwa kwenye kiti chake .
“Mr. Duncan, what is this? (Mr Duncan hiki ni nini?)” alisema Farudume kwa hasira baada ya kugundua mdogo wake ameletwa mbele yake akiwa na Uku-Uku Yule mbirikimo wake.
“Consider this a plan B. now it is you who gonna find us our treassure, we will be watching you full time. (hesabia hii kama Plan B. sasa hivi ni wewe ambaye utaenda kututafutia hazina yetu, tutakuangalia muda wote),” alisema Mr. Duncan na kumfanya Farudume apande hasira baada ya kuona mambo yamemgeukia.

Kumbe wakati wamemuita Farudume afike hapo ofisini wao walikuwa wamemzunguka kwa nyuma muda mrefu na kuwateka Uku-Uku na Eddy pale nyumbani. Lengo ni kwamba walikuwa wamepanga ikiwa Tinonko atasumbua kwa namna yoyote basi pesa zao zisiende bure bali Farudume awe mbadala wa Tinonko.
Hilo ni kutokana na sababu mbili, ya kwanza Farudume ana historia ya kuwahi kufika eneo hilo na kujua namna ya kutoka kwake, lakini la pili waliligundua baadaye kuwa Farudume alikuwa na mbirikimo kutoka Kivu ambaye hasa alikulia katika utajiri huo na ndiye aliyekuwa akimpa ujeuri Farudume kwa kumbashiria mambo mengi ya ajabu.
Sasa wazungu hao wakatumia fursa hiyo kumpiku Farudume, kama kawaida Uku-Uku hakutaka kitu kingine chochote zaidi ya amani na sehemu ya kustarehe, hapa wazungu hao wakamfurahisha kwa kumpa sehemu nzuri zaidi ya Tinonko na kumzungushia wanawake warembo waliokuwa wakimhudumia kwa kila hitaji la roho na mwili.
Uku-Uku akaona hayo ndiyo maisha aliyokuwa akiyahitaji, akalainika na kukubali kufanya chochote hata kumdhuru rafiki yake Farudume ambaye siku zote aliishi naye. Hapo ndipo unaweza kuona uovu wa Uku-Uku ukimfananisha na Aka-Baka.
Wazungu hawa hawakuwa na utani, ndani ya nusu saa Farudume alikuwa nusu kaputi akipandikizwa kifaa cha GPS katikati ya shingo yake karibu kabisa na mshipa mkuu wa damu wa Arteri. Kifaa hicho kiliwekwa hapo ili kisiweze kutolewa kijanja na ikiwa mtu atafanya hivyo basi atajiua mwenyewe kwa kukata kwa bahati mbaya mshipa huo muhimu. Pili kifaa hicho kilikuwa na sumu ya Mercury ndani yake na ikiwa Farudume atagoma kufuata wanachomuelekeza basi hawatasita kumuua.
Meza ikageuka, Farudume naye akapandishwa ndege na kudondoshwa kwenye msitu wa Kongo, misheni yake ni kutafuta sehemu zilizopo mali za Mbirikimo na hiyo itakuwa usalama wake na mdogo wake kipenzi la sivyo atakosa yote. Safari ikaanza ama kweli; mwinda, huwindwa. 


ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.