NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA TATU(43)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.“Hapana siyo wewe?” alisema Aka-Baka.
“Ni mimi,” alisema Aka-Baka wote wakacheka.
“Wengi wanatumia sifa za watu wazuri kuingia katika maeneo yetu, wewe ninashangaa umetumia jina la rafiki yetu mkubwa, Tinonko.. pengine unamfahamu, haya tuambie umetokea wapi?” aliuliza Twa huku akimuoneshea mshale Tinonko kama vile anataka kumchoma nao.
“Hapana msiniue, ndiyo mimi.. tulikuwa wote kumuokoa mtoto wenu kutoka mikononi mwa Ntaganda. Tulikuwa wote mliponipa dawa za mjusi wa bluu na Majani ya Mfalme wa ndege.. ni mimi mliyenipa zawadi ya rubi 81, lulu 60 na almasi za pinki 12,” Tinonko alijikuta akiropoka maneno lakini Twa hakuonekana kushtuka hata wale mbirikimo wengine walianza kumsogelea na mishale yao kama vile wanataka kumuulia mbali.
“Mimi ndiye mwenye mikono kumi!” alipiga kelele Tinonko. Maneno hayo yakamfanya Twa na Aka-Baka washtuke na kuweka silaha zao chini.
Wakiwa katika mshangao, wakaanza kumsogelea ili kumjulia hali kwa yaliyompata, lakini akapiga kelele; “Msinishike!”
Wote wakarudi nyuma na kumtaka Tinonko awaambie nini kinachoendelea hapo ndipo akaanza kuwahadithia kuhusu magonjwa aliyoingizwa mwilini na wabaya wake. Wote wakastaajabu na kuwalaani wabaya wa Tinonko.
Kilichowafanya wajisikie vibaya zaidi ni baada ya kujua kuwa ana siku mbili tu za kuishi na kama wakiamka salama asubuhi basi atakuwa na siku moja tu hivyo ilikuwa ni lazima wamtibie kwa tiba ambazo hawajawahi kuzitumia hata siku moja.
Hapo ndipo Aka-Baka akamtazama Twa na kumwambia: “majibu anayo Achi-Twa,” yaani maana yake anayo marehemu Twa. Kwa lugha nyepesi Achi-Twa ni mfalme aliyepita kabla ya huyu lakini neno Achi lilisimama kwa maana ya mkubwa na marehemu hivyo Twa huyo alikuwa amekufa tayari.

Kilichoanza hapo ilikuwa ni purukushani za kuandaa tambiko ambalo lililengwa kufanyika dakika chache zilizofuatia lakini walikuwa makini kutompeleka Tinonko kwenye kijiji chao kwa kuogopa maambukizi hivyo bila kumgusa wakaanza safari ya kuelekea kwenye kaburi la Achi-Twa.
Kaburi lake lilikuwa limetengwa na makaburi mengine yote kutokana na umuhimu wake. Na baada ya miaka kibao ya kutolitembelea kaburi hilo sasa walifika kwa sababu maalumu nayo ni kuokoa rafiki ambaye japo kuwa hana damu ya kimbirikimo lakini aliacha kumbukumbu ya kuwasaidia kupita maelezo hivyo akawa zaidi ya rafiki kwao.
Wakina mama wa Kimbirikimo walianza kulifagia kaburi la Achi-Twa na kuanza kuimba nyimbo mbalimbali, vilindi vya moto vikawashwa na kufanya eneo zima liwake na kutoa mwanga ulioonesha kila kitu wazi.
Ndipo Aka-Baka akainuka na kusogea kwenye kaburi la Achi-Twa, akaanza kuongea maneno ya ajabu ajabu, kisha akafusha moshi wa vumba aliloliwasha; akazunguka nao kaburi lote kisha akauzima.
Kwa maajabu, ule moshi wote ulipanda na kujirundika sehemu moja. Kisha ukarudi na kusambaa juu ya kaburi kama vile shuka. 
Hapa ndipo Tinonko aliposhuhudia maajabu ambayo hakuwahi kuyaona tangu azaliwe. Akaona ule moshi ukinyanyuka na kuweka taswira kama vile mtu amejifunika shuka. Kisha ukawa na mikono na miguu ukakaa katikati ya lile kaburi na kutoa sauti mbaya mno kwa lugha nisiyoifahamu.
Akasema; “Olatatala Obungu Msweyo!”
Tinonko alishangaa hata alipomuuliza yule mtafsiri wa Aka-Baka alishindwa kumwambia kitu, zaidi ya kusema lugha hiyo anaijua Aka-Baka pekee na si mtu mwingine yeyote kati yao.

Aka-Baka akaanza kuongea na jitu hilo lililotokana na moshi, akaonekana akishindana nalo hoja na mwishowe baada ya nusu saa ya malumbano, likainuka na kuelea angani na kwenda hadi pale alipokuwa Tinonko.
Ghafla likarudi kwa Aka-Baka na kusema naye maneno mengine, tena kisha ule moshi ukasambaratika na kuwa kama moshi wa kawaida ukasambaa na kupotea angani.
Aka-Baka akarudi pale alipokuwa Tinonko akionekana kuchoka na maongezi, akamtazama Tinonko na kumwambia; “pole sana rafiki, umepitia mengi lakini kiini chake leo tumekijua, ila kwanza inabidi ukatumbukie ndani ya mto Kongo mara saba.”
Kwa maneno hayo ilionekana wazi kuwa tambiko lilikuwa limekwisha, Tinonko akajikongoja zake taratibu hadi kwenye mto Kongo ambao ulikuwa jirani na hapo walipokuwa wakifanya matambiko.
Akajitosa na alipoibuka alianza kuona madonda yake yakifutika kama matope, akazama tena na tena alipoibuka mara ya saba, akajiona mzima wa afya kana kwamba hakuwa na ugonjwa wowote.
Akajinyosha mgongo wake uliokuwa ukimuuma kwa mbali ukalia “ko!” na kunyoka kabisa. Kila mmoja kati ya wale Mbirikimo wakamtambua kama ndiye Tinonko hasa.
Wakati huo wote kule kwenye taasisi ya utafiti walikuwa wamejiandaa na kuamua kumfutilia Tinonko kupitia GPS Track ambapo walimpachika mitambo hiyo Tinonko bila kujijua.
Waligundua kuwa Tinonko aliweza kusimama kwa muda mrefu kwenye baadhi ya maeneo. Kwa kuwa walikuwa wakimuona kama kidoti tu kwenye kompyuta hawakuweza kujua alichokuwa akikifanya. 
Wataalamu walitazama haraka zile sehemu na kuvuta picha za Setelaiti na kummulika moja kwa moja pale alipokuwa Tinonko na kugundua alikuwa kwenye moto kule kwenye tambiko, baadaye walimuona akioga kwenye mto na kupona mbele ya macho yao.
Sasa zoezi la mwisho ni kujua wanapoishi wale Mbirikimo na Tinonko alikuwa akielekea huko na walikuwa wakimfuatilia kwa Setelite taratibu.
Je, watu hao watafanikiwa kujua siri za Mbirikimo.

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.