NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA TATU(43)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Wakati huo kule kwenye taasisi ya utafiti walikuwa wakihaha kumtafuta kapteni Tinonko kwa sababu aliivunja kamera yao. Wakawa wanajaribu kutumia GPS kumfuatilia nyendo zake lakini wakati huo wakatuma haraka videge kamera vingine kama viwili hivi ili kumtafuta kuanzia pale mahali walipoishia.
Hadi siku hiyo, Tinonko alikuwa amebakiza siku tatu tu za kuishi na alianza kujisikia tumbo lake likigoma kupokea chakula cha aina yoyote. Wakati huo maumivu yalizidi mara dufu na yale mauvimbe usoni mwake yalimfanya asitambulike kabisa.
Lakini aliendelea mbele bila kujali chochote, akayageuza maumivu yake kuwa hasira, akaigeuza hasira yake na kuwa nguvu za kumuongezea uwezo wa kufika anapopataka.
Ilionekana kama vile hatari zote za wanyama na viumbe wa ajabu wa Kongo walimpitia mbali naye, kwa sababu alivuka mito yenye mamba bila kularuliwa, alivuka majabali yenye simba na chui bila kushambuliwa.
Ilikuwa kama vile dunia yote ilikuwa kimya na ni yeye pekee alikuwa akitembea kama kiumbe hai. Mara alianza kujisikia kizunguzungu kikali, akadondoka chini na kupoteza fahamu kabisa.
Alishtuka mapema kesho yake akiwa palepale chini, mwili wake ukiwa umeanza kutoa harufu na madonda makubwa. Kwa mujibu wa siku zake za uhai, siku hiyo zilikuwa zimebakia siku mbili tu kufikia kifo chake na dalili alikuwa amekwisha anza kuziona.
Maumivu na ugonjwa ulionekana kumtafuna ndani kwa ndani kabla ya kuanza kujitokeza nje. Mathalani ukiongeza na jinsi alivyokuwa amechoka kwa kutembea siku nne mfululizo nako kulichochea kuumwa kwake.
Lakini hakutaka kukata tamaa akajitahidi ili ainuke, alishindwa na kujikuta akidondoka chini tena, akaanza kujikongoja kwa kutambaa japokuwa yalikuwa ni maumivu tosha kwake.


  Asubuhi ya siku hiyo, Farudume alionekana akiwa na wale watwana wake wawili, Peter pekee ndiye ambaye hakuwepo kwenye kikao kile na hilo wote walilishangaa.
  Farudume kwa hasira alianza kuelezea nini kilichotokea. akapanga mashambulizi dhidi ya Peter na yeyote atakayekuwa karibu naye.
  Kifo ndiyo adhabu pekee iliyoamuliwa juu yake, ili kukwepa ushahidi juu ya yote waliyoyafanya. Kwa msisitizo Farudume akataka kazi hiyo iishe haraka siku hiyo ambayo alifahamu fika kuwa ndiyo siku waliyokuwa wakiisubiria kwa hamu yaani siku ya harusi ya Peter na Jackline.
  Gari zikaandaliwa na kuanza safari yake kutoka Dar hadi Morogoro huku ndani yake wakiwa wale makatili wawili ambao kazi yao ilikuwa ni kuwaua Peter, Jackline na Suzy ambaye walinyaka vielelezo vyake mapema kabla ya kuamua kuwafuata.
  Walifika usiku na kuingia moja kwa moja kwenye sherehe wakiwa ndani ya suti kama ndugu waalikwa, hawakutaka kabisa kufanya mauaji kwa njia ya kawaida yaani kuwashambulia watu kwa risasi au silaha nyingine.
  Walitaka kufanya mauaji yao bila kelele yoyote, huku wakitaka kutohusisha kabisa watu wasiohusika na kama watakuwepo basi wawe wachache zaidi. 
  Mpango ukawa ni kuweka kemikali kwenye kitu ambacho kitakuwa karibu na maharusi hata watakapoondoka nyumbani.
  Hivyo wakaweka kemikali yao katikati ya maboksi ya zawadi waliyokuja nayo. Kemikali hiyo si nyingine bali ni ile kisayansi inayoitwa; Azido Azide Azide. Kemikali ambayo ni namba mbili kwa hatari na huhifadhiwa kwenye giza pekee lakini pindi itakapofunguliwa tu na kugusa hewa na mwanga wa kawaida, huripuka na kuweza kusababisha maafa makubwa.
 • Harusi ilifikia kilele chake ambapo watu mbalimbali walianza kutoa zawadi zao, wale makatili wawili wakatumia njia hiyo na kigiza kilichopo kuyapenyesha yale maboksi ya zawadi kwa kuwatumia baadhi ya watu palepale ukumbini.
  Kwa macho yao walioshuhudia Peter na Jackline wakiyapokea, na Suzy akiyaweka kwenye zawadi nyingine walizopewa. Lakini kama kawaida Peter alionekana kuwa na wasiwasi zaidi kuliko kawaida akitazama kila kona ya ukumbi kila mara, Suzy naye halikadhalika.
  Harusi iliisha, maharusi wakaondoka kama walivyopanga safari hii ikawa si kurudi nyumbani bali kwenda fungate na Suzy akiwa kama msaidizi wao huko waendako.
  Ingawa ukweli ulikuwa, Suzy alifika hapo harusini akiwa na dokomenti zote muhimu kama vile, hatimiliki zote za mali za Tinonko ambazo kisheria sasa zitakuwa za Jackline na mumewe Peter. 
  Na siku hiyo ndiyo Suzy na Peter walikuwa wamepanga kumuua Jackline ili kufurahia utajiri wao waliouhangaikia kwa muda mrefu na hatimaye wameupata kwa mbinde huku maisha yao yakiwa hatiani kwa kuhofia mkono wa Farudume.
  ***
  Kapteni Tinonko akiwa anaendelea kusota akasikia sauti ya mtu anayemfahamu ikimuamuru kusimama, akahisi masikio yake yakimdanganya. Akageuka na kutazama kwa mshangao macho yake yakagongana na Aka-Baka na wapambanaji wa Kimbirikimo, lakini hakuwa ameonesha kumtambua.
  Yeye alikuwa akimtambua akamuita; "Aka-Baka!"
  Aka-Baka akaonekana kushangaa akamtazama mtu huyo anayeonekana kuwa na sura na mtazamo mbaya kuliko watu wote wa Kongo.
  "Wewe ni nani?" alihoji Aka-Baka.
  "Kapteni Tinonko," alisema Tinonko akijua fika kuwa Aka-Baka ametatizika na mabadiliko ya umbo lake.

 • ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.