NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI(42)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.“Tulikuwa tunajadili aina ya gauni ambalo unatakiwa kulivaa siku ya harusi kwa sababu ya tumbo lako. Lile ambalo unalitaka nadhani itabidi uliache na tushoneshe jipya,” alijibu Suzy.
“Anha! Sasa mbona mmeangaliana kwa hasira hivyo?” alisema Jackline baada ya kugundua nyuso zilizojikunja.
“Yeye hapa alikuwa anang’ang’ania uvae gauni la kawaida, sasa najua tu kitumbo kitaonekana na hautapendeza au unasemaje?” alijibaraguza Suzy, Peter akaelewa mchezo huo naye akatia neno; “kama utataka gauni jipya utaniambia,” aliongea kisha akaondoka zake.
Usiku Suzy alijisikia vibaya kuonekana msaliti mbele ya Peter akampigia simu na kuomba waonane naye chumbani kwake. Usiku huo Peter kama kawaida akavizia na kuingia chumbani kwa Suzy maana hata yeye mwenyewe alitaka kufahamu kwa nini mwenzake aliamua kumfanyia hivyo.
“Peter naomba unisamehe ni wivu tu ndiyo uliokuwa ukinisumbua, nilikuwa nikiona kama vile umeanza kumpenda Jackline na ukimuoa mimi ndiyo basi tena sitakuwa na nafasi moyoni mwako,” aliongea Suzy.
“Acha upumbavu! hatuwezi kuvumilia yote hayo halafu nikakuruhusu uharibu mwishoni!”
“naomba nisamehe,” alisisitiza Suzy.
“tatizo hujui ulichosababisha, umejitafutia matatizo mwenyewe Suzy,” aliongea Peter huku akimtazama kwa huruma Suzy kiasi kwamba alizidi kumchanganya.
“nimejisababishia matatizo kivipi? Kwani hautaki kunisamehe au?” “Siyo kwamba sitaki kukusamehe, lakini ….” Alisita kuzungumza Peter.
“kuna nini naomba niambie,” alisema Suzy.
“Suzy, najua tumefahamiana kwa muda mrefu sana, na tumekuwa tukifanya dili nyingi, lakini haujawahi hata siku moja kujiuliza ishu zote hizi nazipataga wapi?
“Watu wenyewe wana nguvu mno,” alisema Peter.

“Sasa hao watu wanahusiana nini na mimi na wewe?” alijikuta akiongea kwa wasiwasi Suzy.
“Ulichokifanya leo ndiyo kimekufanya wewe na mimi wote tuwe hatarini, kwa sababu watu ninaofanya nao kazi ni … Yaani nashindwa nisemeje lakini ni watu siriaz sana kifo kwao si kitu. “Wewe fikiria, mpango mzima wa kumuua Tinonko ulifanywa na wao na hawataki chochote na hizi mali zote wameniachia mimi, hebu waza kwa akili yako ni watu wa aina gani?”
“Peter mbona sielewi?” alianza kuogopa Suzy.
“Ulivyokuwa ukinitisha kwa zile meseji, niliamua kumpigia bosi na kumueleza, haraka akatumia watu wa mtandao na kujua simu hiyo kuwa ipo hapahapa nyumbani.
“Kwa sababu maneno uliyokuwa ukiyaandika hakuna mtu yoyote anayejua nje ya duara zaidi yako, ndiyo maana nikakushuku, hapa wanachokitaka ni kujua nani aliyekuwa akitishia kutoa siri na mbaya zaidi wanataka nimuue,” alihitimisha Peter.
“sasa kama usiponiua je wao watajuaje?”
“haujui unachokiongea mpumbavu wewe! kazi zetu ni lazima turudishe ripoti, bosi ana macho na mdomo nchi yote hii, anajua kama anadanganywa na anajua kama anaambiwa ukweli, sijui anajuaje lakini nisipokuua lazima ajue?” aliongea Peter.
“Peter kwa hiyo tunafanyaje mbona unanitisha?” aliongea Suzy kwa hofu.
“kinachoniumiza kichwa ni kwamba bosi lazima atake kujua mtu huyo alijuaje kuhusu mipango yetu na kama alikuwa nyumbani kwangu basi ndiyo kabisa atahisi kuwa mimi ndiyo niliyemwambia, kwa hiyo kifo siyo chako tu hadi kwangu.”
“Sasa kwanini ulimwambia kuhusu zile meseji,” alianza kuangusha kilio Suzy.
“Acha ujinga! si nilikuwa nikikuuliza kila mara, ulitegemea siri nzito kama hiyo nifanyeje, zaidi ya kumpiga bosi?”
“sasa tunafanyaje?” aliuliza Suzy kwa hofu.

“Siwezi kukuua, inabidi tusubiri kifo,” alisema Peter akionesha kukata tamaa.
Wakati huo ndiyo simu ya Farudume ilikuwa ikiingia; kama walivyozungumza, Farudume aliuliza maswali hayohayo; “Mtu huyo ni nani?”
“Kwanini alikuwa nyumbani kwa Peter?”
“Nani aliyevujisha siri hizo kwake?”
“Je, amemuua au bado?”
Maswali hayo yote yalikuwa yakitakiwa kujibiwa na mtu ambaye si mwingine bali ni Peter ambaye alijikuta akibabaika kama vile hakujiandaa.
Mbaya zaidi alijua adhabu ya mtu kuvujisha siri za kazi zao hakuna nyingine zaidi ya kifo, hivyo akakosa majibu na kuishia kukata simu ya Farudume kitendo ambacho kilitosha kabisa kuonekana msaliti.
“Suzy umeharibu Suzy!” alilalama Peter.
“Sikia Peter cha msingi kwa sababu harusi ni keshokutwa muoe huyo kinyago wako na ukishamaliza tu ndoa, tukombe mali zote na tupotee kabisa hapa,” alisema Suzy jambo ambalo kidogo lilionekana kuleta amani kwa Peter japokuwa alijua ni ndoto kuifikia kesho.
“Sikia Peter, huyo mtu ulisema hataki chochote zaidi ya kumuumiza Tinonko na wewe akakupa ruhusa uchukue mali zake na umuoe mkewe, inabidi ufikirie kwa nini alikwambia ufanye vitu hivyo kwanza,”
“kwanini?”
“cha kwanza anaonekana ana hela nyingi sana, lakini cha pili inaonekana anakutumia wewe ili umuumize Tinonko kwa kuharibu familia yake. Kwa hiyo hawezi kukuua hata kidogo hadi pale utakapomuoa, sasa ukimaliza tu ndoa tunaondoka na kila kitu,” alisema Suzy maneno yaliyomuingia akilini Peter akatuliza akili japo kuwa sura ya Farudume ilikuwa ikimjia kila saa katikati ya mawazo yake.

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.