NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THELASINI NA MBILI(32)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Lakini hata hivyo kabla hajaondoka Sajenti Ngowi aligeuka na kumuuliza Peter; “Koplo hivi kumbe unakaa hapa?”
“Aah ..ehe ndiyo mkuu,” alihangaika kunyoosha maelezo Peter wakati huo Jackline alikuwa amepigwa na butwaa baada ya kugundua kumbe Peter alikuwa ni mwanajeshi.
Mawazo hayo ya Jackline yalipotezwa na kelele za simba aliyebweka kwa sauti na kumfanya Peter aliyekuwa akimtazama Jackline kwa jicho la pembeni aamue kukimbilia ndani.
“Peter.. mbona sielewi nini kinachoendelea hapa. Wewe na wale wanajeshi mnajuanaje?” aliuliza Jackline kwa ukali.
“sikia Jackline ni tofauti unavyodhania, unamkumbuka Saidi yule rafiki yangu mwanajeshi?” alianza kutunga uongo Peter.
“sasa yule jamaa mara nyingi sana alikuwa akinichukua na kuingia kambini kwao, si unajua kule kuna bia za bei rahisi na hata vitu vya supamaketi zao ni bei rahisi sana japo kuwa wanauziwa wanajeshi peke yao.
“sasa Saidi alikuwa akinichukua na tukawa tunaenda pale kambini na mimi nikijifanya mwanajeshi ili nisigundulike. nilifundishwa salamu zao ndiyo maana nilikuwa na uwezo wa kuongea nao vizuri.
“huyu jamaa aliyekuja ndiye mtu aliyekuwa amenizoea pale kambini na kujua kama mimi ni mwanajeshi kweli, ndiyo maana hata alivyoniona hapa ameniuliza hivyo. Ndiyo maana na mimi niliamua kujifanya ni mwanajeshi ili nisiharibu mambo,” alimaliza Peter.
“ha! nilitaka nishangae mwanajeshi gani hadi saa hivi uwe nyumbani. Halafu wanajeshi mimi hata sitaki tena mambo ya kuishi na mapresha kila saa siyataki,” alisema Jackline akionekana kukubali uongo mtakatifu aliopewa na Peter.

Huko nyuma, Farudume alikuwa makini kusikilizia matokeo ya mambo aliyoyafanya, baada ya muda ndiyo akasikia yule mbwa alikuwa ameuawa kwa kupandisha kichaa kule uwanjani, akafurahi kuwa kazi yake imeisha.

Lakini ghafla furaha yake ilikatishwa na simu kutoka kwa Peter akisema; “Mkuu nimekutwa na Sajenti Ngowi nyumbani kwa Mamba (tinonko).”
“Unasemaje! Alikuja kufuata nini?” “Walikuja kumrudisha mbwa wa Mamba hapa nyumbani kwake wakati huo mimi sikujua nilikuwa nimetoka nje ndiyo wakaniona.”
“mbwa wake? Mbona ameshauliwa leo.”
“hapana, yupo hapa nyumbani na ameanza kunisumbua.”
“unanichanganya Peter, rudi kambini haraka!” Alitoa amri Farudume huku akionekana kuchanganyikiwa kwa kile alichoambiwa muda mchache uliopita.
Ili kuhakikisha kama kweli yule mbwa siyo, akaamua kutoka nje na kwenda moja kwa moja hadi kule alipofanya yale mambo yake, akaamuru wale waliompiga yule mbwa risasi wamuonesha mzoga wake.
Alipouona akagundua kuwa siyo yule aliyemkusudia. Akili yake ikamkumbuka Sajenti Ngowi ambaye alionana naye asubuhi, akakumbuka maneno aliyoambiwa na Peter muda mchache uliopita kuwa alimuona sajenti huyohuyo nyumbani kwa Tinonko.
Akaona mtu huyo ni kikwazo ambacho kinatakiwa kudhibitiwa mara moja. Akapiga simu kwa wale watu wake watatu ambao siku zote huambatana na Peter kwenye vikao vyao vya siri.
Ndani ya maongezi yao akawataka wakamilishe kazi moja muhimu, ambayo ni kummaliza Sajenti Ngowi haraka sana kwa kuwa hakutaka kuacha alama yoyote itakayompa mashaka na kusababisha kuanza kuwafuatilia.
Kapteni Tinonko akiwa katika chumba chake bado akiwa hajui nia ya watu waliomteka, ukimya na siku zilizidi kusonga na hilo lilimchanganya.
Ukimya ulimnyong’onyesha na kujihisi mfungwa. Akamkumbuka sana mke wake, akamkumbuka mama yake, hasira zilimpanda lakini ghadhabu zake ziliyeyuka kama theluji.
Tofauti na siku alizokaa humo, siku hiyo aliona watu wakiingia ndani kwake kama kawaida huku wakiwa wamejificha nyuso zao kama maninja, kisha wakampiga picha Tinonko, walipomaliza wakaondoka zao.
Hakujua picha hizo zilikuwa za nini lakini alikuwa na uhakika kuwa mtesaji wake alikuwa na kitu alichotaka kuzifanyia.


***
Nyumbani Jackline aliagana na Peter aliyeonekana anawahi sehemu ambayo kama kawaida alimficha, mimi na wewe tunafahamu kuwa sehemu hiyo si nyingine zaidi ya Jeshini alipoambiwa arudi haraka na Farudume.
Peter haraka akapanda pikipiki na kuelekea nyumbani kwake, akabadilisha mavazi yake na kuvaa kombati za jeshi kisha akapanda tena ile pikipiki kuelekea kambini. Wakati huo kuna mtu alikuwa akimpiga picha kupitia simu yake ya mkononi naye akapanda pikipiki na kumwambia dereva amfuatilia Peter.
Wakati huo mtu huyo ambaye hajulikani alimtazama simu yake ikiita na kuipokea kisha akazungumza na mtu wa upande wa pili; “nimemuona ndiyo.. amevaa magwanda na yupo kwenye pikipiki anaelekea kambini kwake.”
“Kwa hiyo kweli ni mwanajeshi?” alizungumza mtu huyo wa upande wa pili.
“ndiyo anavyoonekana, ila asilimia zote nitakupa kama tu nikimuona akiingia ndani ya geti lao,” aliongea mtu yule aliyekuwa kwenye ile pikipiki kisha akaiweka simu yake mkononi na kuitazama pikipiki ya Peter ikiishia getini. Naye akaingia ndani bila kujua kama kuna mtu anamfuatilia.


ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.