LIVERPOOL YAIZAMISHA CHELSEA NYUMBANI KWAO KATIKA DIMBA LA STAMFORD BRIDGE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Timu ya Liverpool imeendeleza kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuiharibia rekodi Chelsea ya kutofungwa katika msimu huu, kwa kuipa kipigo cha magoli 2-1 katika dimba la Stamford Bridge.

Katika mchezo huo Liverpool ambayo mchezo uliopita iliwafunga mabingwa watetezi Leicester City kwa magoli 4-1, ilianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kuandika goli kupitia Dejan Lovren na kisha Jordan Henderson akaongeza la pili.

Beki wa Chelsea, aliyenunuliwa kwa paundi milioni 32, David Luiz, akiichezea Chelsea kwa mara ya kwanza akichukua nafasi ya John Terry ambaye ni majeruhi alisaidia Chelsea kupata goli moja kupitia kwa Diego Costa.
                            Jordan Henderson akifunga goli la shuti la umbali wa yadi 30
                      Diego Costa akipongezwa baada ya kuifungia Chelsea goli pekee 
Post a Comment
Powered by Blogger.