DK. SHEIN AFANYA ZIARA ATEMBELEA NA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA SEHEMU MBALIMBALI UNGUJA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Idara ya Uvuvi katika Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Nd,Mussa Aboud Jumbe Mwinyi wakati alipotembelea Eneo lilatakalojengwa Soko la samaki,Malindi Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiuliza suala kwa Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Kapteni Abdalla Juma (mwenye kipaza sauti) wakati alipotembelea Eneo la chelezo Malindi wakati akiwa katika ziara maalum ya kutembelea lilatakalo jengwa Soko la samaki,Malindi Mjini Unguja.
Baadhi ya Akina Mama wanaofanya bishara ya kuuza chakula katika maeneo ya Bandari ya majahazi wakimuangalia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Ujumbe wake wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati pichani) akiwa na ujumbe aliofuatana nao wakati alipotembelea katika maeneo ya Bandari ya majahazi alipofanya ziara ya kutembelea maeneo hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Msimamizi Mkuu wa mradi wa Ujenzi wa Hoteli ya Bwawani (STONE TOWN VILLAGE LTD) Syed Mansour Hussein alipotembelea ujenzi wa Hoteli hiyo leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Msimamizi Mkuu wa mradi wa Ujenzi wa Hoteli ya Bwawani (STONE TOWN VILLAGE LTD) Syed Mansour Hussein alipotembelea ujenzi wa Hoteli hiyo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ pia Mshauri wa Rais Mambo ya Uchumi Mzee Abdulrahman Mwinyi Jumbe wakati akiangalia ramani za ujenzi na kutembelea Eneo litakalojengwa Ofisi za Benki ya Watu wa Zanzibar Malindi Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na Viongozi baada ya kutembelea Eneo litakalojengwa Ofisi za Benki ya Watu wa PBZ Malindi Mjini Unguja jana.
 (Picha na Ikulu)
Post a Comment
Powered by Blogger.