DIAMOND NA DAVIDO BADO SANA KWA “SAAD LAMJARRED” MSANII WA AFRIKA ANAYEONGOZA KWA NYIMBO ZAKE KUTAZAMWA ZAIDI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Saad Lamjarred ni msanii mkubwa wa Morocco, ambaye namba zake zinatisha – ni balaa kabisa. Hii ni kwa sababu macho mengi uwafuatilia wasanii wa Nigeria pamoja na wasanii wa Afrika ya Mashariki bili kutazama kwa upande wa Afika ya Kaskazini kwenye nchi kama Morroco, Misri na Algeria.
Kwanza ana followers milioni 3.5 Instagram. Hiyo inafuta kile tulichokuwa tunaamini kuwa, Davido ndiye mwanamuziki wa Afrika mwenye followers wengi zaidi kwenye mtandao huo (2.9m) akifuatiwa na Diamond (2.7m) huku Wizkid akiwa na 2.5m.
Video yake mpya, GHALTANA ilitoka August 25, lakini hadi sasa imeangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 36. Kama hiyo haitoshi, video ya wimbo wake, LM3ALLEM iliyotoka May 2, 2015 ina zaidi ya views milioni 390.
LM3ALLEM uliingia kwenye kitabu cha Guinness World Record kwa kupata views milioni 100 ndani ya miezi mitatu. Ni video ya kiarabu iliyotazamwa kuliko zote.
Nyimbo zake “Mal Habibi Malou” na “Machi Sahel” zimevutia views milioni 161 na milioni 66 kwenye Youtube hadi sasa.
Post a Comment
Powered by Blogger.