MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » YUSUPH KIKWETE AWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA MIDDLE STAR SALOON FOUNDATION


Pamoja Blog 8/30/2016 05:57:00 PM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mgeni Rasmi akipeana mikono na Afisa Habari na Masoko,James Mbuligwe,kulia ni Katibu Msaidizi Wilaya, Salumu Mtelela.
Mgeni rasmi akiwa mteja wa kwanza kunyolewa baada ya kuzindua.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Ccm Taifa Yusuph (katika) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi na wateja baada ya kufungua rasmi Middle Star Saloon Bagamoyo.

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (Nec) Yusuph Mrisho Kikwete amekuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Middle Star Saloon Foundation iliyopo Wilaya ya Bagamoyo,Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo Leo,Mjumbe huyo wa kamati kuu Nec ambaye aliongozana na Katibu msaidizi wa wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Salumu Mtelela amesema kuwa wameamua kuunga mkono kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

?Nimefurahishwa sana kuona vijana wanaamua kujiajiri haswa katika kipindi hiki ambacho nchi mbalimbali duniani zinapitia changamoto za ukosefu wa ajira kutokana na ongezeko la watu, kilichonifurahisha zaidi licha kuwa saloon ni ya kisasa lakini huduma zake za chini mtu yoyote anaweza kumudu,amesema Kikwete.

Kwa upande wake Mkuu wa habari na Masoko wa Foundation hiyo,James Mbuligwe amesema kuwa lengo kubwa ni kufungua Saloon katika maeneo mengi ndani na nje ya mkoa ili vijana watumie nafasi ya kujiajiri kupitia kunyoa nywele .

?Saloon moja inachukuwa zaidi ya watu 10, hivyo ukiwa nazo 10 unakuwa umesaidia vijana zaidi ya 100 kuajiriwa ndio maana tumeamua kufungua mradi huu na leo tutatoa huduma bure kwa siku nzima ili kila mmoja apate ofa hii lengo letu ni kupunguza tabia hatarishi zilizokuwepo katika jamii yetu zikiwemo utumiaji wa Madawa ya Kulevya ,Ukahaba na Ujambazi.

Mbulingwe amesema kila mtu anawajibu wakulinda amani ya nchi na kijana akikosa kitu cha kufanya ni rahisi kuingia kwenye makundi mabaya

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments