WASANII WA BONGO FLAVA UDE UDE NA IQU JUNIOR WAFARIKI DUNIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Marehemu Ude Ude wa kushoto na rafiki yake Iku ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo
Msanii na mtunzi wa nyimbo za Bongo Flava, Hamid Hafidh maarufu kama Ude Ude na rafiki yake Iku wamefariki dunia wakiwa mkoani Tanga.
Akiripoti kuhusu tukio hilo kwenye kipindi cha Papaso cha TBC, rapper Baghdad amesema kuwa chanzo cha kifo cha marehemu bado hakijawekwa wazi lakini taarifa za mwanzo zinaeleza kuwa msanii huyo alifikwa na mauti yeye na rafiki yake wakiwa katika tukio linalosadikiwa kuwa ni la kijambazi na inaelezwa kuwa marehemu na wenzake wamekuwa wakijihusisha na matukio hayo mara kwa mara kwa kivuli cha heshima waliyonayo kwenye jamii.
Iqu Junior amewahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake ‘Nisamehe.’

Marehemu Ude Ude alijipatia umaarufu kwenye muziki wa Bongo Flava kwa umahiri wake wa utunzi kwa kuwaandikia nyimbo wasanii mbalimbali. Nyimbo alizozitunga ni pamoja na ‘Wangu’ wa Lady Jaydee, ‘Maneno Maneno’ wa Queen Darleen, Ulofa by Top C, ‘Bwashee’ ya Baby J, ‘Oyoyo’ ya Bob Junior na zingine kibao. Wimbo wake ulioweza kuhit ni Ngoma Inogile – waweza kuangalia video yake hapo chini.

Wasanii mbalimbali wametoa salamu zao za rambi rambi kwa msiba huo akiwemo Z-Anto aliyeandika:
Miongon mwa vtu vbaya katka maisha ya binadam ni kuisema maiti, hakuna ajuae mwisho wake hakuna ajuae chanzo cha umauti wake, waweza kuwa mcha mungu lakin chanzo cha umauti wako ikawa ni zinaa, au uongo, ama wizi, ama utapeli, ama lolote ambalo hukuwah kulifanya ama kulitarajia ndio maana tunaambiwa ktk vtabu vyetu tunapaswa kujiombea kupata mwisho mwema, wangap walikuwa ni wenye dhambi hawamjui mungu wao pengne walikuwa vchochez wa vtu vbaya lakin nia zao za mwisho zkawafanya wapate mwisho mzur wa maisha yao kama watu waliofariki makka walipokwenda kuhiji, so tusipoteze muda kuzisema maiti kwan cc pia ni maiti watarajiwa na hatujui mwisho wetu, tusemeni, inna lillah wainna ilaih Rrajiuun/bwana ametoa na bwana akatwaa
Post a Comment
Powered by Blogger.