MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » USAIN BOLT ASHINDA MEDALI YA DHAHABU YA MITA 100


Pamoja Blog 8/15/2016 08:09:00 PM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ameandika historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda medali ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio za mita mia moja, kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio 2016.

Bolt, 29, ametumia muda wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika michezo ya olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya Olimpiki mjini Beijing 2008, na London 2012.

Gatlin, ambaye amepigwa marufuku mara mbili kwa matumizi ya dawa za kusisimu misuli, alimaliza sekunde 0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.
“Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda,” Bolt ameiambia BBC.
Mwanariadha wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake.
Bolt anatazamia kuondoka Rio na medali zaidi za dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi ilivyokuwa katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.
Mwanariadha huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa dunia mwaka 2017.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments