UPDATES: MSANII MKONGWE WA MUZIKI WA TAARAB, BI. SHAKILA SAID AFARIKI DUNIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab, Bi. Shakila Said amefariki dunia usiku huu katika Hospitali ya Temeke jijini Dar. 

Habari zilizotufikia muda huu kuwa Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia usiku huu muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Shani ambaye ni mtoto wa mwisho wa marehemu ameithibitishia kuwa Bi Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya
 kumaliza kuswali alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alikokimbizwa  alikutwa amekwishafariki.
Taarifa za kifo cha msanii huyo nyota mwenye umri wa miaka 70 zilianza kusambaa mitandaoni usiku, na kuhanikiza katika redio mbalimbali ambazo zilianza kucheza muziki wa mkongwe huyo ambaye wakati wa uhai wake alibahatika kuzaa watoto 15, 12 wakiwa hai.
Kwa mujibu wa taarifa za kifo cha mtunzi na mzimbaji huyo wa nyimbo wa kundi la JKT Taarab, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo ukisubiri taratibu za mazishi. Shakila alianza muziki mwaka 1961 akiwa na umri wa miaka 15. 

MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA

Sikiliza moja ya nyimbo alizotamba nayo
Post a Comment
Powered by Blogger.