NEYMAR AIPA BRAZIL MEDALI YA DHAHABU KATIKA MICHUANO YA OLIMPIKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Neymar amefunga penati ya ushindi wakati wenyeji Brazil wakiifunga Ujerumani kwa magoli 5-4 kwa mkiwaju ya penati Jijini Rio na kushinda medali yao ya dhahabu ya Olimpiki katika mchezo wa soka wanaume.

Katika mchezo huo mkali timu hizo zilijikuta zikitoka sare yagoli 1-1 baada ya muda wa nyongeza, huku goli la mpira wa adhabu lililofungwa na Neymar likisawazishwa na Max Meyer.

Ushindi huo wa Brazil umekuja baada ya Ujerumani kuichakaza Brazil magoli 7-1 mwaka 2014 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Duniani katika dimba la Belo Horizonte nchini Brazil.
                                   Neymar akifunga mpira wa penati ulioipa ushindi Brazil
Neymar akishangilia goli kwa kuonyesha ishara inayotumiwa na mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt
         Mwanariadha wa Jamaica Mfalme wa Riadha Usain Bolt akifuatilia mchezo huo.

Nayo timu ya taifa ya Nigeria imeshinda medali ya fedha katika michuano ya Olmpiki ya soka la wanaume baada ya kuichakaza bila huruma timu ya Hondura kwa mgoli 3-0 yaliyofungwa na Sadiq Umar mawili na Aminu Umar moja.
Post a Comment
Powered by Blogger.