NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA SABA(7)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Japo kuwa walikuwa na hatua za kitoto lakini sura zao zilionekana walikuwa watu wazima wasio na mchezo hata kidogo na kile walichokuwa wakikifanya.
Wakiwa wanaingia ndani ya himaya yao mara walitokea mbirikimo wawili wanene zaidi ya wale waliokuwa wamewakamata mateka, wakaongea maneno wasiyoyafahamu lakini kwa kuongea kwao wakajikuta wakifunguliwa kamba na mmoja baada ya mwingine wakanyweshwa maji fulani machungu mno.
Ilionekana kama vile maji yale yalikuwa yana dawa kwa akina Tinonko na wenzake maana baada ya kunywa tu kila mmoja wao alianza kuhisi kurudiwa na nguvu kwenye misuli yao.
Wakiwa wanatafakari juu ya tendo hilo, nyuma ya chaka kubwa alitokea Aka Baka akiwa ameketi juu ya kobe mkubwa mno, akazungumza na akina Tinonko lakini hakuna mmoja aliyeelewa nini anasema.
Katika muda huo akaletwa mtafsiri wa Mfalme Twa, mmoja wa mbirikimo waliyewahi kuishi maeneo machache ya Tanzania na kufahamu lugha ya Kiswahili kwa mbali. Akaanza kutafsiri kwa akina Tinonko yale yaliyokuwa yakisemwa na mganga mkuu zaidi, Aka –Baka.
“Ilioneshwa kwetu kuwa mutu mukubwa kutoka mashariki atakuja kutuokoa!” alizungumza yule mtafsiri wa Kimbirikimo akiwaambia akina Tinonko walioanza kumwagiwa mafuta ya majani ya mnyonyo kuwa ishara ya kuwakaribisha watu wenye heshima kijijini kwao.
“Mtakua mmekosea! sisi ni wanajeshi kutoka Tanzania, tumepata ajali tukiwa tunarudi nyumbani,” alisema Komando Niko na hivyo ndiyo ilikuwa kwa kila mtu kati yao hata yule Rubani wa ndege yao.
“Mungu wetu hawezi kudanganya, alisema naye mutu mkubwa atakuja na mikono yake kumi,” alisema yule mtafsiri baada ya kusikiliza maneno ya Aka- Baka.
“mwambie mimi nina mikono miwili tu, hiyo mikono nane iliyobaki ipo wapi? Alijibu Niko  Wakati huo Kapteni Tinonko alikuwa amejikausha kimya.

Yule mtafsiri alimnong’oneza Aka-Baka kisha naye akamjibu kitu yule mtafsiri ambaye alicheka sana.
“Aka-Baka anasema kumbe ukubwa wa mili yenu ni tofauti na akili zenu?” Kwa maneno haya, Komando Niko akakaa kimya kwa aibu kwa kuwa alijua neno mikono kumi kumbe ni fumbo, hapo ndiyo Komando Tinonko akajitokeza kama mkubwa wao akamwambia yule mtafsiri; “Mwambie Aka-Baka tunaomba atuelekeze njia rahisi ya kutoka katika pori hili.”
Kwa sauti ile Aka-Baka akasimama juu ya mgongo wa yule kobe mkubwa na kumtazama Kapteni Tinonko huku ametumbua macho, akasema maneno yasiyoeleweka.
Mara wale askari wa kimbirikimo wote wakarudia maneno yaleyale huku wakimtazama Tinonko. Akiwa ameduwaa kwa tendo hili la ajabu mara msitu mzima ukawa kama vile umeingiwa na uhai, maelfu ya mbirikimo wakina mama na watoto, wakajitokeza na wote wakazungumza neno moja.
Kapteni Tinonko alijikuta akishindwa kusubiri tafsiri ya jambo lile akamkamata yule mtafsiri na kumwambia haraka amueleze maana ya kitendo kile, naye kwa woga akasema; “Aka-Baka anasema wewe ndiye mwenye mikono kumi na ndiye utakayetusaidia.”

Ilikuwa ngumu kuwaelewa mara moja lakini moja wa wale mbirikimo aliyekuwa karibu na huyo Aka-Baka aliinuka na kuchukua jiwe jekundu mfano wa madini ya Rubi kisha akalipitisha kwenye kundi zima la makomando wa Tinonko, lakini alipofika kwa Tinonko likawaka mfano wa taa , ghafla palepale wote waanguka chini na kupiga magoti.
Ni jambo la kushangaza lakini baada ya hayo wakajikuta wakikaribishwa kwa ukarimu mkubwa na kupewa vyakula vya kila aina na kuhudumiwa kama wafalme. Hawakuelewa lakini wakaapa kutulia tuli ili wasiwakasirishe wenyeji wao.
“Kapteni, hawa watu wanakuona wewe ni Mungu wao,” alisema Komando Seba na kila mtu akacheka isipokuwa Kapteni mwenyewe ambaye mawazo yake yalikuwa nyumbani kwake ambapo kadri jua lilivyozidi kuzama ndivyo moyo wake ulizidi kuzizima.


>>>

Huko nchini Tanzania, habari za ndege ya kivita kupotea angani zilisikika kila kona ndani ya makao makuu ya jeshi. Na kwa kifupi ilikuwa habari mbaya zaidi.
Taarifa hizo zilipenya pia na kuvifikia vyombo vya habari lakini uthibitisho wa wanajeshi hawa kuwa ni wazima au wamekufa ilikuwa bado ni mtihani. Ndege za kivita za Umoja wa Mataifa na zile za Tanzania zilipiga doria angani kutwa kucha lakini hawakuweza kupata chochote kwa wakati huo zaidi ya kuona misitu mikubwa isiyoisha.
Unaweza ukavuta picha habari hiyo mbaya ilipomfikia mama yake Tinonko kuwa nini kilimkuta, au pengine nini kilichomkuta Jackline.
Ukweli ni kwamba, kasumba hiyo iliishia kwa mama Tinonko kupata presha iliyompelekea kupooza upande mmoja na laiti kama asingewahishwa hospitali huenda angefariki mara moja.
Lakini kadri siku zilivyozidi kusonga na matumaini ya kuwapata akina Tinonko nayo yalififia, Suzy ambaye ni dada yake Peter, mpenzi wa zamani wa Jackline akatumia nafasi hiyo ya upweke wa Jackline kumkumbushia penzi la kaka yake hapo ndipo mimba ya Tinonko ikawa hatiani kunyofolewa na nafasi yake ukatungwa ubaya na ukazaliwa. Je, Tinonko akirudi atafanya nini zaidi ya kulipa kisasi.


ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.