NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THELASINI(30)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 • Suzy akiwa na presha ya kupata msala akahangaika kumbeba shoga yake aliyeongezeka uzito mara dufu kutokana na kuwa mjamzito.
  Akampa huduma za kwanza, ikiwemo kumpulizia pumzi kinywani lakini kama haitoshi akamkandamiza kifuani na kuhakikisha amemvua nguo zote zinazobana. Lakini yote hayo alikuwa kama vile anatwanga maji kwenye kinu, mambo yalipomzidia alimua kumuita mlinzi haraka ambaye naye baada ya kuona bosi wake akiwa katika hali hiyo alichanganyikiwa.
  Hapo ndipo ghafla taksi ilisikika ikipiga honi nje na Peter aliingia ndani haraka wakambeba mgonjwa wao hadi hospitalini kwa huduma stahiki.
  Baada ya takribani nusu saa ya madripu na huduma nyingine, Jackline alifungua macho yake usiku huo na kugongana uso kwa uso na Peter aliyeonekana muda wote amejilalia kwenye kiti kilichopo jirani na kitanda.
  Kumuona Peter akiwa pembeni yake, kidogo kulimpa ahueni. Baadaye akajua kuwa alikuwa amezimia kwa presha, tatizo lililoonekana kumkabili sana kipindi hiki cha ujauzito wake ambao taratibu ulianza kufikia miezi mitano.
  “Peter,” aliita Jackline kwa sauti dhaifu ya kigonjwa.
  Peter akashtuka katika usingizi na kumtazama Jackline akasimama haraka na kwenda pale alipokuwa amelala.
  “vipi mpenzi unaendeleaje?” aliuliza Peter akijua madhara ya mchezo waliomfanyia Jackline muda mchache uliopita ambao moyoni Peter alitaka mara moja uishe.
  “najisikia uchovu tu, kwani ulikuwa wapi tangu asubuhi?” aliuliza Jackline.
  “nilikuwa bize sana kazini yaani hata muda wa kuwa na simu sikuwa nao, hadi usiku aliponipigia simu Suzy,” alijibu Peter.

 • “Wewe mwanaume utaniua,” alisema Jackline kiutani lakini moyoni akijua ni kweli kabisa alichokizungumza.
  “hapana siwezi kukufanyia hivyo hata siku moja,” alisema Peter na kumshika mkono begani Jackline.
  “Unajua Peter nimefikiria sana na nimeona tuoane tu haraka na tuondoke kabisa hapa Dar,” aliropoka Jackline.
  “Mh! Usinitanie bwana,” alisema Peter.
  “nimeamua hivyo na nitawaambia wazazi wangu najua hakuna wa kupinga kwa kuwa wananitegemea mimi kwa kila kitu,” alisema kwa uhakika Jackline.
  “sasa na hii mimba itakuwaje?”
  “hii niachie mimi kwa sababu sioni kama kuna tatizo nikijifungua wakati nikiwa naishi na wewe,” “Lakini hilo suala la ndoa ni jambo la kufikiria sana Jackline sio kwamba ukaja kujutia uamuzi wako,”
  “hapana nimeamua hivyo na sitakuja kujutia chochote,” alisema Jackline uamuzi ambao sote tunajua ulichochewa na wivu na maneno aliyoambiwa na Esteria kwa hiyo plani ya Suzy ilikuwa imetiki.
  Peter kwa wakati huo akawaza na kuona hakuna tabu kwa kuwa hata kama atamuoa Jackline na kuishi naye nyumba moja hakutakuwa na tatizo akiwa na mimba yake kwa kuwa yeye atakuwa na haki za mali zote kama mume na hapo sasa ndiyo kwa kuweza kufanya chochote ikiwemo kumteketeza Jackline kama alivyokuwa amepanga.
  Haraka akamtaarifu Farudume ambaye alikubali na kumpongeza Peter kwa kufikia hatua hiyo huku akisisitiza kuwa yeye hataki chochote kutoka kwa Tinonko zaidi ya kumsababishia maumivu makubwa, fedha na mali zote akimwachia Peter na wenzake.
  Unaweza ukajiuliza kwanini mtu kama Farudume alikuwa na kisasi dhidi ya Tinonko kwa kiasi hicho, lakini ukweli huenda anaujua mwenyewe na ipo siku utakuja kujulikana wazi.
 • Farudume akiwa katika ubora wake aliwahi kazini alfajiri kuliko wafanyakazi wote akihakikisha kila kitu kinakuwa salama kabla ya kupiga hatua yake kuelekea kule kwenye kitengo cha mbwa wa jeshi.
  Akili yake ikiwa moja kwa moja imelenga kukamilisha zoezi la kumfanya mbwa Simba kusahau kuhusu bwana wake yaani TInonko kwa kuwa moja kwa moja alijua aliyefuatwa na mbwa hapo si Peter kama alivyojishuku bali alikuwa ni Tinonko.
  Mbwa huyo ina maana alikuwa amenusa harufu ya Tinonko kwa umbali mrefu na ndiyo maana alikuwa amemfuata katika eneo hilo, hivyo hofu ya Farudume ilikuwa kama mbwa huyo angemwachia basi angeweza kuibua siri kuwa Tinonko kuwa hapo kambini na suala hilo hakutaka litokee mpaka mipango yake kwanza itimie.
  Akiwa anapiga hatua za uwizi akafika kwenye moja ya mabanda ya mbwa na kugundua kuwa kuna banda moja la wazi lilikuwa nje huku kukiwa na mbwa aliyefungiwa ndani yake.
  Mbwa huyo alionekana wazi kuwa ni simba kwa kuwa alikuwa na rangi na umbo kama vile ambavyo Farudume alikuwa ameambiwa hapo awali na Peter. Hivyo haraka akachukua ule unga wake alioufungasha kwenye koti lake la kijeshi na kuumwaga akizunguka lile banda.
  Akamaliza zoezi hilo na kuanza kupiga hatua akirudi alipotoka, lakini ghafla Sajenti Ngowi aliyekuwa akiingia akagongana uso kwa uso na bosi huyo mkubwa wa kitengo tofauti na yeye. Sajenti Ngowi akampigia saluti akajiuliza ni jambo gani bosi huyo alikuwa ametoka kulifanya lakini hakuweza kuling’amua.
  Mara baada ya Farudume kuondoka ndipo Sajenti Ngowi aliweza kugundua kitu mfano wa Unga wa njano na hatua za mtu zikiwa zimezunguka banda la mbwa lililokuwa karibu na alipo. “Mh! bosi mwanga? Haha..hapana sasa haya maajabu! ina maana siku hizi anarogwa mbwa na si mwanadamu tena,” aliongea kimoyomoyo Sajenti Ngowi huku akicheka.
  Sajenti Ngowi amegundua alichokifanya Farudume 

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.