NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TATU(3)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kapteni tinonko akiongoza kikosi cha brigedi ya watu kumi na mbili, walitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kinshasa, wakipokelewa na msafara wa vifaru vya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Japokuwa wakati huo jua lilikuwa likizama kuashiria mwisho wa siku hiyo, Kapteni Tinonko aliweza kugundua nyuso za wanajeshi hao zikionekana kuchoka kwa vita isiyokoma kutoka kwa waasi wa M23. 
Ingawa walipowatazama wakina Kapteni Tinonko na wenzake kutoka Tanzania, wanajeshi hao walionekana kupata hamasa na morali wa kupambana.
Tinonko na wenzake walifahamu hiyo ilitokana na umaarufu wa jeshi la Tanzania kwa weledi wake vitani kwa kuwa halijawahi kushindwa vitani kwenye historia yake hata siku moja. 
Hivyo kuitwa kwao kwenye misheni ya wiki moja nchini humo ilikuwa ni heshima kubwa na kuliongeza hamasa kwa wanajeshi wa Congo na wanajeshi kutoka nchi nyingine.
Hakukuwa na usafiri mwingine kutoka hapo Kinshasa zaidi ya kupanda malori makubwa ya jeshi la Umoja wa Mataifa hadi mjini Goma ambapo ndiyo makao makuu ya majeshi ya Umoja wa Mataifa.
Waliambiwa kuwa wakifika Goma ndiyo watapangiwa wapi kwa kuanza kazi, safari hiyo ilitajwa kutumia masaa nane wakiwa barabarani tu kutokana na ubovu wa barabara na madaraja. 
Bila kusahau kuwa njiani watalazimika kupitia kijiji cha Bunagana kilichotekwa na waasi wa M23 ambapo lazima mapigano yangetokea hivyo wakaweka tahadhari ikiwemo Kapteni Tino kuandaa kikosi chake kiwe tayari kwa lolote.Wakiwa njiani kwenye safari hiyo ndefu, kapteni Tinonko akaanza kuyakumbuka yaliyotokea saa chache zilizopita akiwa Tanzania, ni ngumu kumuaga mke aliyetoka kumuoa dakika chache tu.
Akamuwaza mama yake aliyeonekana kukosa furaha kabisa na hata kufikia kusema maneno ya kujutia mwanaye kuingia jeshini. Ni kazi nzuri lakini linapokuja suala la vita mara nyingi inahitaji moyo kuwaaga uwapendao.
Lakini pia akamkumbuka mbwa wake kipenzi, Simba. Akakumbuka huenda kuwa hata kule kubweka kwake sana jana yake pengine kuliashiria jambo baya litakalotokea, na huenda jambo lenyewe likawa ndiyo hili la kusafirishwa ghafla kwenda vitani kwenye siku mbaya kama hiyo.
Lakini kama mwanaume aliyaweka yote hayo kifuani na kubeba bendera ya nchi yake, akijipa moyo kuwa amepewa heshima kubwa, kuongoza kikosi cha taifa lake. Hasa akifikiria kuwa misheni yenyewe ni ya wiki moja na kurudi, hivyo ataweza kurudi na kuendelea na maisha yake, lakini neno ‘Mungu akipenda’ likapita akili mwake.
Akaona lazima kabla ya kujipa uhakika wa kurudi amuachie Mungu kwani yeye ni mpangaji wa yote. Kwa kuwaza hayo akachomoa rozali yake aliyoivaa kifuani na kuibusu kisha akairudisha.
Vitani mara nyingi kila mtu huwa na kitu chake anachokiamini, wengine huwa na hirizi kubwa, wengine wanabeba vitakatifuzi vya dini zao kama vile Kapteni Tino.
Ghafla aligutuka kutoka mawazoni baada ya kusikia mirindimo ya risasi hewani, hapo ndiyo akasikia sauti ya wale wanajeshi wenyeji zao wakipiga makelele; “Mutu ya Temineta Ntaganda imevamia kwa bele yetu, piga risasi ua!”

Kapteni Tinonko na wanajeshi wake haraka wakashuka na kuweka fomesheni ya kivita maarufu kama Roman Infantry Tactic, wakiwa na bunduki zao aina ya SMG Colt- Model 635, bila kupoteza muda wakaingia uwanja wa kivita.
Japo kuwa ilikuwa ngumu kwa giza lile kutazama walipojificha maadui lakini kwa tekniki ya kutazama moto wa bunduki unapotokea waliweza kugundua walipojificha maadui zao na kujibu mashambulizi.
Kwa ujuzi mzuri wa kulenga shabaha waliweza kufanikiwa kuwashinda maadui zao huko na kuwafanya wengi wakimbie mapambano huku wakipiga makelele; “mujeshi ya Tanzania! Mukibie sasa!”
Katika mapambano hayo walifanikiwa kukamata waasi waliosalenda vita zaidi ya kumi na nane, japo kuwa wao nao wanajeshi wenzao watatu waliumizwa vibaya na risasi. Waliwabeba na safari ya kuelekea Goma ikaanza huku njia nzima wanajeshi wenzao wakiwapongeza kwa ujasiri wao.
Walifika kambini usiku mno na moja kwa moja walikutana na kamanda wa Vikosi vyote vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa nchini Kongo, Luteni Jenerali, Emille Jansens aliyetangulia kusikia uhodari wa kikosi cha Kapteni Tinonko.
Mzungu huyo aliyeonekana kuwa na maneno machache, alimsalimia kwa heshima Kapteni Tinonko na kumkabidhi misheni nzima, huku akiwaonesha maturubai ya kulala sambamba na silaha za kazi.
Hapo wakitakiwa kuyazoea mazingira kwa siku mbili kabla ya kuanza kazi rasmi iliyowapeleka nayo si nyingine bali kumkamata kiongozi katili wa waasi wa M23, Bosco Ntaganda ambaye maarufu kwa jina la ‘Temineta’ neno la kiingereza lenye maana “Muuaji”
ITAENDELEA ALHAMISI

Post a Comment
Powered by Blogger.