NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO(25)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Akiwa ameingia ndani ya jengo hilo lenye utulivu na ulinzi wa hali ya juu, simba alijikuta akishindwa kujificha, ghafla mlinzi mmoja akapiga kelele akimuita mwanaume aliyejulikana kwa jina la Festo. Naye akaja haraka akiwa na wenzake na kumfunga Simba kisha wakatoka naye nje na kwenda kumuingiza katika jengo lililojaa mbwa wengine wengi.
Sehemu hii, simba aliijua vyema ndiyo sehemu ambayo alizaliwa na kukulia hata baada ya kuonekana hana sifa zaidi za kuwa mbwa wa jeshi na kuchukuliwa na Kapteni Tinonko bado hakuisahau sehemu hii. Aliwatambua mbwa wenzake ambao walikuwa wamevalishwa medali na vyeo mbalimbali na kuonekana wana nguvu na misuli imara kuliko yeye ambaye alionekana tipwatipwa.
Kwenye tundu la nondo alilofungiwa akakaa kimya na kuonekana mnyonge, yote ikiwa ni wasiwasi wake juu ya bosi wake, Tinonko. Maana tayari mlango wake wa ishirini wa fahamu ulishathibitisha yupo hai na yupo ndani ya jengo hilo ndani ya makao makuu ya jeshi.
Hata hivyo suala la mbwa kuingia ndani ya jengo aliloingia simba lilikuwa na matokeo yake kwa kitengo cha mbwa ambacho kilitakiwa kuwajibika kwa makosa hayo, mara kadhaa mbwa hutoroka kutoka kwenye eneo lao la mafunzo na huenda sehemu mbalimbali lakini si ndani ya jengo hilo.
Hivyo mkuu wa kitengo cha mbwa alipaswa kupewa adhabu ikiwemo kukatwa mshahara na kutakiwa kufanya lindo usiku kwa wiki mzima. Akiwa amejiona mwenye bahati mbaya kupata adhabu kwa uzembe wa walio chini yake akarudisha hasira zake kwao.


Moja kati ya vitu alivyovitamka kutoka katika ulimi wake ni kumtafuta mbwa huyo kwanza na kuhakikisha anapokea viboko arobaini ili asirudie kosa, lakini kwa wale walinzi wa kitengo hicho waliomwachia mbwa atoke kiholera nao walionja joto ya jiwe kwa kutakiwa kukesha nje na bosi wao. 

Haraka mwanajeshi wa cheo cha chini kabisa katika kitengo hicho akatoka na kuingia katika eneo lile la mbwa, haraka akamkokota Simba hadi katika uwanja wa adhabu na kumfunga barabara kiasi cha kushindwa kutoroka. Kisha mkwaju ukaandaliwa. 

Lakini kabla hajafanya chochote alipaswa kumwambia mbwa huyo kosa lake, kwa kuwa mbwa hufundishwa kwa kuoneshwa kosa lao kwanza, vilevile hupewa zawadi kwa kuoneshwa kitu chema walichofanya, simba pia alioneshwa kosa lake. 

Sajenti Omary jasho likimtoka akamuonesha Simba lile jengo na kumwambia kama anaongea na mwanadamu mwenzake, “hautakiwi kufika kule umesikia! Pumbavu.” 

Akanyosha mkwaju wake juu na kuuvurumisha juu ya mgongo wa simba kwa hasira na kwa nguvu, sauti ya maumivu ya mnyama huyo ikasikika, akavurumisha ya pili nayo ikatua palepale. Kwa kelele alizopiga mbwa huyo alionekana hawezi kufikisha mikwaju arobaini. 

Kwa kawaida mbwa wote walio kwenye mavunzo kwenye eneo lile huishi kwa sheria kali zinazowaongoza na pindi wakivunja sheria hizo, viwango vya bakora huzidiana kwa kila adhabu lakini ikiwa mbwa ataadhibiwa viboko arobaini basi hapo huwa ndiyo kiwango cha mwisho wa adhabu. 

Japo kuwa pamoja na adhabu hizo, hapo jeshini kuna matunzo mazuri kuanzia chakula na hata matibabu, mbwa koko wa kawaida anayezunguka mtaani huenda ana ndoto za kuingia jeshini na yeye kuwa mwanajeshi wa jeshi la mbwa ambalo nalo lila vitengo na vyeo. Majeshi mengine huwa na farasi, na wengine nchi za mbele huwa na hadi jeshi la panya, nyuki na viumbe visivyotamkika. Yote hayo ni kujiandaa na vita na mambo mengine zaidi. 

Sauti ya Simba alisikika zaidi na zaidi lakini mpigaji hakuchoka kwa kuwa alikuwa na hasira ya kupata adhabu iliyomuuma sana yaani kupewa lindo la usiku mzima. 

Siku hiyo, Peter aliyeona bahati kuiona akiwa hai, alimwita Suzy faragha na kumwambia kila kitu, kuanzia kuhusu alivyonusurika kuuawa na Farudume na mengine mengi lakini jambo kubwa likiwa ni suala la Kapteni Tinonko yaani mume wa Jackline kuwa hai. 
“haiwezekani yupo wapi?” aliuliza Suzy kwa wasiwasi. “yupo hapahapa mjini, lakini Faru ana mpango wa kumuua kabisa,” alisema Peter. 

“Kama hivyo sawa! lakini inabidi hata na sisi tumalize kazi yetu haraka kama alivyosema la sivyo, tutasherehekea kuzimu,” alisema Suzy na kumpa mipango Peter. 

“Sasa wakati huu hebu niachie mimi mwanamke mwenzake. tena kama vipi inabidi nimtafute msichana mwingine amtie wivu, maana najua anakupenda lazima akisikia unazengewa, atasema mwenyewe umuoe,” alisema Suzy na haraka akampigia simu shoga yake Asteria. 

“Sasa wewe kazi yako inabidi umtietie wivu huyu mdada, ila chondechonde ole wako utembee na Peter wangu,” alisema Suzy na kumpa onyo Peter pia kwa kuwa alijua wanaume si watu wa kuwaamini kwa marafiki wa kike wa karibu. 

Peter akafurahi kuona mpango unawezekana kukamilika kwa ujanja wa Suzy, akarelax na muda huohuo, Jackline akaingia sebuleni kitumbo chake kikionesha kuanza kuweka uvimbe wa kuashiria mjamzito, hilo liliwakera wote na hata Jackline mwenyewe lakini hakuwa na cha kufanya kwa sababu mara ya kwanza mpango uligoma. Hivyo siku hiyo walikuwa wamepanga kwenda kwa daktari mwingine huko Tandika na safari hii Peter mwenyewe alikuwa anaongoza msafara.

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.