NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE(24)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ama kweli mtu mwema ndiyo hutangulia kufa siku zote na siyo jitu baya maana yasemekana eti Mungu humuacha mtu mbaya aishi muda mrefu ili apate nafasi ya kutubu dhambi zake.

Mfano mzuri ni Nyerere na Nduli Iddi Amini, Nyerere alikufa mapema wakati Iddi Amini alizeeka kabisa. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Peter ile risasi iligoma kutoka na mlio ukawa; “Click”.
Ilikuwa wazi kuwa kile chuma cha ile triga kilikuwa kimepiga tundu lisilokuwa na risasi, hiyo ndiyo ikawa salama yake ambayo hata Peter mwenyewe hakuamini.
“Kijana unaonekana una bahati sana. Sasa hii haitatokea tena tutakapokutana mara nyingine,” alisema Farudume akiirudisha ile bastola yake mfukoni.
“Nakupa mwezi mmoja nataka nione yote tuliyoyapanga yanatimia, hakikisha mke wa Tinonko anaitoa mimba na unamuoa!” alisema Farudume kwa ukali kiasi cha kumfanya Peter aitikie huku akitetemeka na kwa uoga sana.
Akiwa amenusurika kuuawa siku hiyo akarudi nyumbani kwa Jackline akiwa na mawazo kibao, Jackline alimtazama mpendwa wake na kumpokea kwa heshima zote, lakini kuna kitu kilionekana kumchanganya hivyo Jackline akamuachia nafasi peke yake na kuacha kumsumbua kwa lolote mpaka pale atakapokaa sawa.
Akiwa amelala kitandani ndipo Jackline akaanza kuyarudia mambo yaliyomtokea mapema siku hiyo, akahisi kuna jambo linaloendelea kutokana na vitendo vya Simba, akasimama na kukumbuka vizuri jambo.
Akafungua kabati la Kapteni Tinonko na kuchukua albamu yake na kuchambua baadhi ya picha. akagundua picha za zamani za marehemu mumewe, ndani yake akagundua picha nyingine akiwa na huyo mbwa wake.


Picha hiyo ilionekana imeandikwa mwaka 2010, ni miaka michache kabla ya yeye kukutana rasmi na Tino na kuanza uhusiano wao, na alikumbuka kuwa hata walipoanza kuishi pamoja, alimkuta mbwa huyo akiwa katika nyumba hiyo na siku zote Tinonko mwenyewe alikuwa akimhudumia vizuri na kukaa naye kwa upendo kama vile alikuwa ndugu yake.
Mara zote akiwa kwenye mazoezi asubuhi huondoka na mbwa wake huyo na kuzunguka naye hivyo mbwa huyo alikuwa ni kumbukumbu tosha, lakini sasa hayupo tena nyumbani.
Na hata hilo suala la mbwa huyo kutajwa kuwavamia hospitalini ndiyo hasa lililomtisha na kumfanya aingie hofu hasa akiwaza, alipajuaje. Wazo la pengine mbwa huyo alikuwa akimlinda kutokana na kutoa mimba lilipita kichwani lakini hakuweza kuamini mbwa anaweza akawa na akili kiasi hicho.
Akajiuliza kwanini simba alikuwa mkali sana kwa Peter na Suzy, akahisi pengine kwa sababu watu hao ni wageni, lakini sababu hiyo ilikosa nguvu mara moja alipokumbuka kipindi fulani aliposhuhudia wageni wengi wakija nyumbani hapo lakini Simba hakuwa na akiwashambulia kama hivyo.
Akiwa na maswali mengi, Jackline akarudi kitandani na kulala, Peter aliyekuwa amejilaza na mawazo alipitiwa na usingizi mzito mapema mno. Akawa kama vile anaweweseka na kuongea maneno ambayo Jackline alielewa mara moja kuwa mwenzake alikuwa akiweweseka.
Mara alimtaja Suzy mara akawa anamtaja mtu anayeitwa Farudume na la mwisho lililomshangaza Peter ni kulitaja jina la Simba huku akipiga makelele kama vile anamshambulia.
Jackline alimshtua mara moja Peter alikagutuka kutoka kwenye ndoto hiyo ya kutisha kisha akalala tena safari hii usingizi mzito.
Huko mtaani alionekana Simba akizurura huku na huko akipanda vilima na kuvuka barabara, kila mtu akishangaa mbwa mkubwa kama huyo akiwa katikati ya jiji.
Tofauti na mbwa mwingine, huyo alionekana ametokea familia yenye matunzo kutokana na usafi wake na jinsi alivyonenepa, shingoni alikuwa na kola rangi ya manjano yenye medani. 
Inasemekana mbwa siku zote huwa na uwezo mkubwa sana wa kunusa harufu, mbwa huyu alikuwa kama vile amechanganyikiwa akaongoza njia na kushika barabara ya Alhasan Mwinyi kisha mbele ya Kituo cha Polisi cha Salenda akaingia kulia na kuelekea makao makuu ya Jeshi, Ngome.
Kila alivyokuwa akikimbia aliongeza spidi kwa kuwa harufu ya Tinonko ilionekana kuwepo katika eneo hilo, mbwa huyo alipita kizingiti cha geti kinachosimamisha magari na kunyoosha moja kwa moja hadi kwenye eneo fulani kisha akasimama na kunusanusa chini.
Eneo hilo ndiyo lile ambalo Tinonko na wale wanajeshi wawili walikuwa wameuawa kwa risasi na Tinonko kupoteza fahamu, Simba akanyoosha kwa spidi hadi mwisho wa uwanja na kuelekea kwenye jengo moja lililopo mbele yake lililokuwa na ulinzi mkubwa mno.
Humo ndiyo harufu ya Tinonko ilizijaza pua zake akazunguka jengo hilo bila kuona wapi pa kuingilia asionekane. Akatikisa mkia kuashiria amethibitisha kuwa anayemtafuta yupo humo akarudi kwenye sehemu ya mlango wa umeme wa kuingilia kwenye chumba hicho na kuusukuma kwa kichwa chake mara ukafunguka kwa kuingia ndani.
Harufu ya Tinonko ikizidi maradufu.


ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.