NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA(21)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Kama mnanijua kwa nini mnanifanyia hivi?” aliongea kwa maumivu makali Tinonko, wale mabedui walimtazama mmoja wao akachukua nyundo na kumfuata akianza kuponda kidole chake cha mkono wa kushoto.
“Sema!” alisema mtu huyo katili akimwambia Tinonko.
“niseme nini?” Tinonko aliongea huku akipiga kelele kwa maumivu makali.
“Tumesikia unatumiwa kuiangamiza Tanzania na Temineta Ntaganda, tena umepewa madini ya thamani kwa ajili ya kazi hiyo. Sasa unachotakiwa kufanya ni kutuelezea mwanzo hadi mwisho kuanzia mlivyokutana, hadi ulipokuja na parachuti na kutua hapa usikuusiku na kuwaua walinzi wetu wawili,” alisema mmoja wa wale watu kiasi cha kumchanganya Tinonko.
“Mimi, nimeua kivipi?” aliuliza huku akiwa anatetemeka hakudhania kama kuja kwake kambini hapo kumekuwa mkosi kwake, lakini lazima kuna mtu atakuwa amepanga kufanya haya ili kumharibia sifa yake nzuri kwenye jeshi la Tanzania, taswira haikuwa ya mtu mwingine bali ni ya yule mwanajeshi aliyemuona siku ile sura yake ikiwa nusunusu.
Baada ya kujua hilo akaamua kukaa kimya kwa sababu alijua hata aseme nini hakuna kitakachomuokoa kutoka kwenye gundu alilolikwaa, akatulia na kuvuta kumbukumbu nzuri za maisha mazuri aliyoyapitia ili kupooza maumivu ya mwili aliyokuwa akipatiwa na wale watesaji.
Yote haya ni ukaidi wake wakutosikiliza Aka-Baka alichokisema lakini hata hivyo hakujutia sana zaidi ya kumeza machungu yote na kuyahifadhi kifuani mwake kwa kuwa alijua amekaribia hatua chache sana ili kumjua mbaya wake.

Asubuhi na mapema, Jackline aliamka akiwa na nguvu na furaha kubwa moyoni, mwenyewe akijua hiyo imetokana na kuwa karibu na Peter hasa baada ya kulala naye usiku mzima nyumbani kwake suala ambalo lilikuwa ni ndoto na haikuwahi kutokea kwenye kipindi chote cha mahusiano yao.
Sasa alijisikia hana majuto wala kubanwa na kitu chochote akaona kwa nini asijiachie. Ladha ya mapenzi ya Peter yalimfanya amsahau kabisa Tinonko na mwenyewe alifurahia sana hilo na kujiapiza kutokubali penzi lake na Peter liingiliwe na mtu yoyote.
Kifupi alitaka kukubaliana na Peter kwa kila kitu likiwemo hilo suala la kuolewa naye, akianzia na suala la yeye kuamua kabisa kutoa mimba siku hiyo, kisha kuwataarifu wazazi wake kijijini kuhusu hayo masuala ya ndoa. 
Akafumba macho kuvuta picha ya jinsi watakavyopokea suala hilo lakini akaona lolote liwe hakuna kitakachomzuia.
Wakati huo Peter alijiandaa kuondoka huku akimtaka Suzy amsindikize Jackline kutoa mimba siku hiyo ikiwa ni mwanzo mzuri wa dili lao kukaa sawa.
Peter akiwa anakumbuka vyema sakata la mbwa jana yake usiku, aliuelekea mlango kwa tahadhari huku akihakikisha Jackline anamsindikiza hadi getini ambapo mlinzi alionekana ana wasiwasi kweli.
“Mama, shikamoo!” alisalimia mlinzi huyo kwa kujihami.
“marahaba , vipi mbona hivyo?” alijibu na kuuliza Jackline.
“Mama Simba ameruka ukuta jana usiku sijui ameenda wapi,” aliongea mlinzi akijua pengine atakatwa mshahara wake kutokana na jinsi marehemu bosi wake, Tinonko alivyokuwa akimthamini mbwa huyo.
“Ha! Sasa wewe ndiyo una wasiwasi kuhusu hilo! Usijali we endelea na kazi zako, kwanza mbwa mwenyewe matatizo tupu humu ndani,” aliongea Jackline jambo lililomfanya Peter naye ashushe pumzi ya afueni akitamani mbwa huyo agongwe na gari na afe moja kwa moja ili aweze kuingia na kutoka ndani ya nyumba hiyo anavyotaka.
Peter akiwa anafikiria hayo mara simu yake iliita, akamuaga Jackline kwa kumbusu pale getini na kuondoka haraka huku akipokea simu kwa wasiwasi na heshima akisema;“Hallow, Koboko,” “Mamba karudi,” ilisikika sauti nzito ya upande wa pili wa simu.
“Nani! haiwezekani? Karudi lini!” alihoji Peter.
“Una bahati tumemdhibiti maliza haraka Faru dume anakusubiri wewe tu!” “sawa, nitafanya hivyo,” alijibu Peter kwa hofu akaweka simu yake mfukoni.
Moyoni mwake akitafsiri kuwa Mamba ni Kapteni Tinonko, Faru dume ni bosi wake mwanajeshi ambaye anawapaga dili nyingi za hatari kama hizo yeye pamoja na wenzake. Huenda ndiye mwanajeshi yuleyule katili aliyemshambulia Tinonko.

***
Saa moja baada ya Peter kuondoka, Suzy na Jackline wakajiandaa kuelekea kwenye zahanati ya Dokta Malienge, daktari maarufu mitaa ya Manzese Tiptop anayejulikana kwa shughuli za kuchoropoa mimba.
Daktari huyo anasifika kwa kumaliza kazi zake haraka na zaidi anatajwa kuwa msiri na mcheshi kwa wateja wake bila kusahau kuwa ana mtandao mkubwa wa polisi ndiyo maana amekuwa na jeuri ya kufanya chochote anachokitaka.
Wawili hao walitoka nje na kukodi gari na kuondoka, lakini nyuma yake Simba aliyekuwa amejilaza nje ya ukuta akawaona na kuwafuatilia nyumanyuma akikimbizana na gari bila Jackline wala Suzy kumuona.
Haikuwa kazi ngumu kwa sababu ya foleni nyingi jijini Dar lakini hata hivyo, wawili hao walifika hadi kwenye zahanati yao na kushuka wakaingia ndani, Simba akiwa nyuma yao bila kujua, tena akatangulia kuingia ndani kupitia mlango wa uani ulioachwa wazi.
Je, Jackline atatoa mimba? Kwanini Simba amewafuata kwenye zahanati hiyo?


ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.