NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA KUMI NA SABA(17)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.“Huyu mtu ni nani?” aliuliza Tinonko akiwa amechanganyikiwa. Angekuwa hajayaona mauzauza ya mwanzo kutoka kwa mbirikimo hao asingeamini, lakini kwa aliyoyaona akashindwa aanzie wapi kukataa kuwa anayoyaona ni uongo.
“Sijui ni nani! ila anaonesha anakujua vyema na mbaya zaidi anaonekana anaujua uwezo wetu ndiyo maana kila nilipojaribu kumvuta sura yake mawasiliano yetu yamekuwa yakikatika,” alijibu Aka-Baka.
“Kwa hiyo hiyo ndiyo sababu unaniambia nisirudi nyumbani? Hapana nitarudi na kuhakikisha kila aliyenitendea ubaya nitafanya malipizi!”
“sikukatazi lakini tunaona hautaweza kufika nyumbani kabla haujafa, na kwa mazuri uliyotufanyia tungependa angalau uwajue kwanza wabaya wako wote ndiyo uweze kufanya maamuzi aidha urudi mapema kama unavyotaka au usubiri kidogo,”
“Hapana lazima nirudi nyumbani, siwezi kuvumilia mke wangu akiwa na mwanaume mwingine na mama yangu akiwa anakaribia kufa hali mimi ni mzima,” alisisitiza Tinonko jambo lililomfanya Aka-Baka aache kuendelea kumshawishi tena na kukubaliana naye kuwa siku hiyo jua litakapozama watatimiza ahadi yao ya kumrudisha Tinonko nyumbani.
Wakiwa wanazungumza hivi, mara kile kitambaa kikafunguka tena, safari hii kikaonesha kaburi la kijeshi lililoandikwa jina lake Capten Tinonko Masato, kisha mbele yake yakawa majina ya makomando wake wale kumi. “Kwa hiyo wanajua nimekufa?” alijiuliza Tinonko kidogo akashindwa kumlaumu sana mkewe kwa kuwa alijua pengine alikuwa ameamua kumsaliti kwa kuwa alikuwa na upweke.

Tinonko akiwa katika mawazo hayo mara akakumbuka mimba yake, akamuuliza Aka-Baka kama anaona chochote ndani ya tumbo la mkewe.
Aka-Baka akafumba macho na kuzungumza maneno kadhaa, Yule mbirikimo mtafsiri akamtazama Tinonko na kumjibu; “mimba ipo lakini ipo hatiani inaonekana mkeo anataka kuitoa.”
Kwa maneno hayo Tinonko akajikuta anadondosha machozi na kumpigia magoti Aka-Baka akimsihi amsaidie kumlinda mtoto wake.
Aka-Baka akachukua mchanga na kuumwaga upande wa mashariki akatazama vumbi likiyoyoma upande wa magharibi kisha likamwagika tena palepale chini taratibu.
“japo kuwa wanajaribu kuitoa na kumuua mama yako lakini nia yao itapotea, mkeo atajifungua na wewe utambeba mtoto wako kwenye mikono yako, lakini si sasa wala baadaye isipo kuwa mpaka ipitapo miaka mitatu.”
Kwa maneno haya Tinonko akajikuta akipoa moyo wake, Aka- Baka akapangusa kile kitambaa chake cha maajabu ghafla akaona mbwa ambaye si mwingine zaidi ya Simba, akabweka kiasi Aka-Baka akafunga kile kitambaa kwa hofu. Akauliza nini maana ya mnyama Yule.
Tinonko akacheka akawaambia yule ni mbwa wake, wote wakatulia kimya wakianza kuhoji kuhusu maana ya neno mbwa na maana yake maana walionekana hawajui chochote kuhusu mnyama huyo muhimu.
Akawaelezea na kuwaambia aina tofauti za mbwa wakiwemo mbwa wa ulinzi, wa kuwinda, wa michezo, na wengine wa urembo.

Basi wale mbirikimo wote wakaonekana wamevutiwa na somo lile wakamuulizia mbwa wa Tinonko ni wa aina gani.
Mwenyewe akajibu kuwa ni wa ulinzi, basi kwa kuwa walikuwa na maswali mengi kuhusu mbwa wake akaanza kuwaelezea jinsi alivyomkuta mara ya kwanza.
Akawaelezea siku ambayo alikuwa anaingia jeshini na kumuona mbwa huyo akiwa kwenye mazoezi sambamba ya mbwa wengine wa jeshi ambapo walikuwa katika mazoezi ya kunusa mabomu.
Tofauti na mbwa wengine Simba hakufaulu mazoezi yote na kushushwa vyeo vya kijeshi ambavyo mbwa wote jeshini walikuwa wakipewa kutokana na uwezo wao katika mazoezi na kwenye matukio.
Tinonko alipomwona mbwa huyu mpweke aliamua kumchukua kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake, hapo ndiyo akagundua kuwa mbwa huyo hakuwa na akili za kawaida kwani alikuwa akiweza kugundua hata nia mbaya za watu.
Aliwasimulia jinsi ambavyo mbwa huyo siku moja akiwa nyumbani kwake alipomvamia muuza urembo aliyeingia nyumbani kwake kumbe alikuwa mwizi tena baada ya kugundulika akiwa na funguo Malaya zaidi ya mia mbili. Akawaambia jinsi mbwa huyo alivyoweza kulia kutabiri siku mbaya kabla hata haijatokea. Akakumbuka jinsi mbwa huyo alivyokuwa akipiga makelele siku yake ya harusi ambayo mwishowe iliishia yeye kutumwa nchini Congo katika misheni hiyo ngumu kuwahi kutokea.
Alipomaliza kusema hivi, kila mbirikimo akajikuta akitamani kupata na yeye mbwa mmoja.ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.