NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA KUMI NA TANO(15)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Kwa harakaharaka, Kapteni Tinonko akagundua kuwa ndiyo maana wale wapiganaji wa kimbirikimo hawana kovu hata moja.
“Aka-Baka, kwa hiyo Temineta Ntaganda ametumia dawa ya kuwa hai ya Muku, sasa ili kumuua tunatakiwa tufanyeje?”
Aka-Baka akacheka na kusema kuwa mwanga wa radi peke yake ndiyo unaweza kumuua mtu aliyetumia dawa hiyo, lakini ikiwa wataendelea kujificha kwenye kambi zao hawatakufa abadani.
Kwa maneno hayo makomando wa Kapteni Tinonko wakanong’onezana kuwa hawatakubali kurudi tena hasa baada ya kuwapoteza rafiki zao katika misheni isiyo na kichwa wala miguu. Wakakataa katakata wakasimama wakiapa kumuacha Kapteni Tinonko peke yake ikiwa atasisitiza kuendelea kubaki.
Mbirikimo waliona uasi huo wa w.ageni wao, lakini Twa na Aka-Baka kwa ukarimu wakawasihi wabaki na kuwaonya juu ya maajabu ya msitu wa Kongo, wakashindwa, ndipo Aka Baka akaruhusu waondoke kwa amani na akawapa zawadi ya madini ya thamani zaidi duniani ambayo yanatajwa kupatikana kwa wingi kwenye msitu wa Sokwe mtu huko Kongo, madini hayo si mengine zaidi ya Ruby.

......................

Siku hiyo mapema Jackline alishtuka na kuketi kwenye kitanda chake akipiga hesabu ya mali alizoachiwa, kuanzia nyumba hiyo kubwa yenye fremu sita alizopangisha wafanya biashara mbalimbali. Akaunti ya benki yenye fedha zaidi ya milioni thelathini ambazo zinazidi kuongezeka kila siku bila kujua nani anayeongeza.
Mbali na hayo nyumba nyingine ambazo bado hakuambiwa na mumewe lakini zilitajwa kwenye mirathi, mashamba za mazao. Mawazo yote haya yakamfanya afurahi na kujiona mjane tajiri zaidi.
Akiwa kwenye mawazo hayo, ghafla Peter akajaa kwenye akili yake, akakumbuka raha walizopeana jana na ahadi walizopeana jana yake. Haraka akaona ni muda sahihi wa yeye kurudiana na mwanaume huyo japo kuwa masuala ya kuoana hakuwa akiyataka kwa kipindi hiki kwa kuhofia ndugu na majirani watamfikiria vibaya.
Hata hivyo alidhamilia kabisa kutoa mimba ya Tinonko kwa sababu alijua kama akiwa nayo atapata tabu kwenye uhusiano wake ujao kwa kuwa alitaka kufaidi maisha ya mahusiano yenye raha na mustarehe na Peter.
Akanyanyua simu yake na kumpigia akimtaka afike nyumbani kwake, tazama Jackline mapenzi yalimzidia akaona amuite hadi hapo nyumbani. Naye Peter bila kuhofia akaahidi angekuja haraka huku naye akimpigia simu mpenzi wake Suzy mapema na kumtaarifu juu ya wito huo na kumsisitiza aweke wivu wa mapenzi pembeni muda wote atakaokuwa nyumbani hapo na Jackline.

Ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi alicholala mama yake Kapteni Tinonko, Dokta Aquinas anaingia na moja kwa moja na kuangalia maendeleo ya mgonjwa wake aliyemuacha jana yake akiwa anaendelea vyema kiafya kutokana na matibabu aliyompatia.
Ghafla anagundua hali tofauti ya mgonjwa wake, presha imeshuka kwa kiwango cha kutisha, hata kuhema kwake kumepungua anaita manesi na haraka wanamsaidia kumpa huduma ya kwanza ikiwemo kushtua mapigo yake ya moyo kwa mashine za umeme lakini hali inaendelea kudorora.
Dokta Aquinas anagundua uwepo wa bomba la sindano na kichupa cha dawa asiyoijua pembeni ya kabati, anashtuka na kuwauliza manesi, lakini hakuna hata mmoja wao aliyejua kuhusu vitu hivyo. “Nani anaweza kufanya unyama huu,” alizungumza Dokta Aquinas baada ya kugundua dawa chupa ile ni syrup ya Ammonia, sumu ambayo husababisha ugonjwa uitwao Hyperammonemia na kumfanya mgonjwa apoteze fahamu na hatimaye kufa kama akiwa hajapatiwa huduma mapema.
Nje anaonekana mwanaume wa makamo aliyevalia kidaktari anaondoka hospitalini hapo na kupanda gari aina ya Noah nyeusi, pindi anapoingia tu anavua nguo zake za kidaktari na kupiga simu kwa mtu asiyejulikana na kusema; “Kamanda, Kazi imekwisha! Kisha akakata simu na kuvua yale makoti ya kidaktari kisha akaondoka hospitalini hapo haraka.” Je, mama yake Tinonko atapona? Je, huyo daktari ni nani, na kwanini ana mwita mtu anayeongea naye kwa simu kwa cheo cha Kamanda?


ITAENDELEA JUMANNE

Post a Comment
Powered by Blogger.