NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA KUMI NA NNE(14)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. • “Kwenu huko mashariki tunasikia mmesahau mambo haya muhimu na kuwafundisha watoto wenu elimy ya Wazungu. Sisi tunaamini katika tiba za dawa za miti,” alisema mtafsiri wa Kimbirikimo akinukuu maneno ya Aka-Baka akiwaambia akina Tinonko.
  “Hata kwetu tunazo, tuambie ni nini hasa mlichokifanya kwetu, hadi majeraha yanapona na nini mlichofanya kuweza kutufungua minyororo kwa majani?” aliuliza Komando Niko huku akihakikisha lile donda la risasi kwenye mkono wake likiwa limepotea kabisa bila kuacha hata kovu.
  “Kuna vitu vingi vya kujifunza kwetu lakini kwa hayo mawili ngoja niwaambie tulichofanya. Ni hivi, baada ya jana nyinyi kukamatwa, sisi tuliona njia pekee ni kurudi nyuma kwa sababu adui yetu tulikuwa tumemdharau kama angeweza kutumia ‘Muku’.
  “Muku ni nini?” aliuliza komando Deo aliyekuwa kimya muda wote.
  “Hamjui! Ni dawa inayoweza kumfanya mtu asife hata kama ameshakufa, ndiyo maana hata wale wanajeshi wa Ntaganda unaweza kuwaona kuwa walikuwa wana kila dalili ya kuwa wafu lakini walikuwa wanatembea na kufanya kazi kama watu walio hai,” alifafanua Aka –Baka.
  “Endelea..” alizungumza Kapteni Tinonko akimwambia Aka-Baka.
  “..basi baada ya kurudi nyuma, tuliwatuma baadhi ya maaskari wetu kuchunguza nyinyi mlikuwa wapi, ndiyo tukagundua kuwa mlikuwa mmefungwa kwenye vizingiti na minyororo kwa ajili ya kuuawa. Hapo ndiyo nikatumia dawa zangu kuwafungua minyororo na kuwaponesha,” aliongea Aka-Baka.

 • “Ni dawa gani za ajabu hivyo!” aliuliza Kapteni Tinonko kiasi cha kumfanya Aka-Baka acheke kwa sauti ya juu.
  “Majani tuliyotumia kuwafungulia minyororo ni dawa ya Mfalme wa ndege na ile ya kuwaponesha majeraha ni damu ya mjusi maji wa bluu.” Kwa maneno haya, Komando Deo alionekana kuchanganywa akauliza kwa shauku. Kuhusu habari za mfalme wa ndege na huyo mjusi maji wa bluu.
  Mfalme wa ndege ni ndege mkubwa mwenye rangi ya kahawia, anajulikana kwa kichwa chake chenye chogo kwa nyuma, pwani anaitwa chogo zingwi au fundi chuma. Mara nyingi hukaa katika vijito vya maji baridi.
  Ndege huyu hujenga viota vikubwa mno ambavyo ndani yake ndege wengine wa aina nyingi huweza kuishi, sababu hiyo ndiyo humfanya aitwe mfalme wa ndege.
  Ndege huyu ana uwezo wa pekee wa kutabiri majira ya mvua na kugundua dawa za aina tofautitofauti ambazo macho ya mtu wa kawaida hawezi kuziona. Kwa sababu hiyo basi waganga mbalimbali pindi wanapomuona ndege huyu akiwa amejenga kiota chake hufuatilia nyendo zake na kugundua mambo mengi mno.
  Mfano, ukimuona akiwa amejenga kiota chake na kuona kikiwa na makinda yake, unavizia akiwa ameondoka kisha unapanda na kukifunga kwa kamba mguuni kimoja kati ya makinda wa mfalme wa ndege kisha unatakiwa kuondoka asikuone mama yao kwa kuwa kama akikuona ni hatari zaidi ya kifo kibaya.
 • Mara zote unapomfunga kwa kamba kinda wa mfalme wa ndege, kinda huyo hupooza na kushindwa kula chochote, hali hiyo humfanya mama yao agundue tatizo la mwanaye, haraka huruka eneo la karibu na kuchukua jani fulani kisha atarudi nalo kwenye tundu lake.
  Kwa maajabu akifika humgusa kwa jani pale kwenye ile kamba na kamba hutoka kabisa mguuni pake, hapa unachotakiwa kufanya mapema kesho yake ni kupanda kwenye kiota na kuchukua lile jani na kuutafuta mti wake maeneo ya karibu na lile tundu la mfalme wa ndege hapo utaona hayo majani.
  Aka-Baka akawaambia majani hayo ndiyo alitumia kuwafungulia mnyororo kule kwenye vizingiti.
  Akiwa haamini Komando Freddy Machos akachukua kamba na kumuamuru mwenzake, Niko amfunge mikononi kisha akaomba apatiwe hayo majani ili ashuhudie. Aka-Baka akayatoa na kumkabidhi Kapteni Tinonko, akayagusisha kwenye ile kamba, kamba ikapukutika kama manyoya.
  “Mungu wangu!”
  Na huyo mjusi maji wa bluu?” aliuliza Komando Freddy Machos akiwa anafikicha macho akiwa haamini anachokiona. 
  Mjusi maji wa bluu ni mjusi mdogo anayepatikana pembezoni mwa maji ya mto, ana ngozi laini mno kutokana na kuishi ndani ya maji masaa mengi zaidi kuliko nchi kavu.
  Mjusi huyu ana sifa ya kurudisha viungo vyake hasa miguu na mkia pindi vikikatika, hata majeraha madogo kwake hupona kwa muda mfupi mno. Hivyo ukichukua damu yake na kuikausha kisha ukamnusisha mtu mwenye majeraha ndani ya masaa matatu anapona kabisa. Na hilo nadhani mmeshuhudia kwa macho yenu.
ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.