NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA KUMI NA MBILI(12)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wakati akijiuliza hivyo akajikuta anawatazama wale wanajeshi waasi wa Ntaganda waliomzunguka, akashangaa kuona wote wakiwa na hali kama ya mkubwa wao, yaani kila mtu ana matundu ya risasi huku wengine wakiwa na majeraha mwili mzima na kutoa hadi wadudu lakini cha kushangaza walikuwa hai; kwa kifupi ni kama vile mazombi.
“Tinonko, mimi sifi hata kidogo, na kwa jeshi langu nitatawala Congo yote na nchi zote hata Tanzania,” alisema Ntaganda huku ngozi ya uso wake ikiwa kama vile imeanza kukauka.
“Kitu nimegundua ni kwamba nina zaidi ya nguvu, hata uliponiua kule Kivu na kujua umeshinda, mimi nilikuwa hai, mimi ni Mungu, hahaaa! lakini ngoja tuone kama utaweza ishi kwa mara nyingine,” alisema Ntaganda huku akiamuru wanajeshi wake mazombi wamfunge kwenye uwanja mwekundu.
Haraka bila kuhoji walimbeba hadi kwenye kile vizingiti na kuwafunga kamba akiwa na wale makomando wenzake wanne, tena kuna lile kundi la wale waasi waliowaua kule Kivu ndiyo walikuwa wa kwanza kuweka nadhiri kuwa watawaua kwa risasi mapema kesho yake alfajiri.
Haya yote yalikuwa ni mambo yaliyozidi kumchanganya akili Kapteni Tinonko akajihisi kuingia kwenye ulimwengu wa mauzauza, sasa akaitazama roho yake ikiwa mkononi.


  Jackline na mpenzi wake wa zamani Peter bado walikuwa wakiendelea kuteganategana kimapenzi lakini kwa ulimi wa hila wa nyoka Peter, aliweza kumvuta mtoto wa watu hadi katika mtego wake.
  Kwa akili ambayo haiwezi kuandikika mantiki yake, Peter na Jackline walikubaliana kukodi chumba kwa ajili ya kile walichokiita ni mazungumzo zaidi kuhusu jambo ambalo Peter alidai kuwa amemuitia katika baa hiyo.
  Wakiwa upande wa gesti ndani ya chumba cha selfu Kontena na kiyoyozi Peter akafungua shati lake na kubakia na singleti kisha akajilaza kitandani huku Jackline akiwa ameketi kwenye kona ya kitanda akijiumauma.
  “Enhe huku ndiyo ulisema utanieleza ulichoniitia haya sema basi, mimi nachelewa nyumbani,” alizungumza Jackline kwa sauti ya chini ya kike. “Haa! Hebu na wewe acha kunichekesha, huko nyumbani kwani unawahi nini? egamia hapa kwanza” alijibu Peter na kumchota Jackline mzimamzima na kumvutia kwenye mto mmoja wapo naye akawa amelala wakitazamana.
  “haa hivi bado hiyo singleti yangu bado unayo tu!” alijikuta akiuliza Jackline baada ya kukumbuka ile nguo aliyoivaa Peter.
  “ndiyo ninayo, kwani kuna tatizo?”
  “mbona unazungusha hebu niambie basi ulichotaka kuongea,” alijibu Jackline wakati huo akijifanya anataka kuondoka nyumbani haraka.
  “Jackline unajua ninaona kama vile Mungu amenipa nafasi nyingine kuwa na wewe, unajua tangu vile umeolewa na yule mwanajeshi wako sikuwa na amani hata kidogo. Roho yangu iliniuma kweli lakini ningefanyeje,” alianza mistari Peter.
  “mh,” aliguna Jackline.
  “Kwa hiyo kwa sasa kwa kuwa huyo mtu wako ameshakufa huko Congo naomba unipe nafasi hii ili tuishi pamoja na safari hii sitaki kukupoteza tena hata kidogo, naomba unikubalie basi Jackie,”
  “kweli inabidi nifikirie kidogo, maana si unajua sasa hivi nina ujauzito na pale nyumbani nina mgonjwa,” alisema Jackline aliyeonekana akianza kulainika vilivyo kwa maneno ya Peter.
 • “Lakini mimi sioni kama kuna tatizo Jackline, mimi ninachohitaji ni mapenzi yako tu na si kingine,” alisema Peter.
  “Sawa lakini.. naomba nifikirie kidogo basi,” aliongea Jackline wakati huo joto la mwili wake likizidi kuongezeka baada ya Peter kuonekana akiwa hodari wa kumpapasapapasa mke wa mtu maeneo f’lani.
  “Peter acha basi… mi.. si..taki mwenzio!” aliongea Jackline kwa sauti ya kukata roho huku Peter akizidisha utundu wake maana alikuwa akiijua vilivyo ramani ya mwili wa mpenzi wake huyo wa zamani.
  Mambo yao yakaishia pabaya kuyaandika lakini mara nyingi inasemekana eti; wapenzi wa zamani wanauwezekano mkubwa wa kupewa penzi kirahisi na wapenzi wetuu kuliko unavyofikiria. Sijui kwanini niwaachie nyinyi wasomaji.
  Saa zilizidi kukatika na jua likaanza kupotea kwenye anga la Mashariki, Suzy akiwa na simu yake aliendelea kufanya yake, hadi wakati huo hakuwa amempa mama yake Tinonko chochote.
  Hali ya mgonjwa ikazidi kuwa mbaya lakini hakukuwa na mtu wa kumjali, ni kama vile aliachwa afe.
  Taratibu akanyata hadi chumbani kwa shoga yake na kuchukua ile bahasha yenye karatasi za mirathi na kuzipiga picha maelezo yote na kila kurasa kisha akazirudisha na kumtumia kaka yake.
  Wakati huo mbwa yule mkali akaanza kubweka zaidi huko nje, Suzy akazidi kupekuapekua vitu kadhaa chumbani kwa shoga yake, na kugundua kadi za kliniki za mahudhurio ya mjamzito. Akaipiga picha kisha akatabasamu hadi mwisho.
  “Mwisho wa umasikini umeshafika, hahaa pole Jackie,” alisema Suzy na kurudi pale sebuleni akajikausha kimya. Sasa makelele ya Simba nayo yalitulia.

 • ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.