MWANAFUNZI WA UDOM AUAWA NA WATU WASIOJULIKANA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka baa.

Tukio hilo limetokea jana usiku eneo la Chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akigalagala njiani.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa, amesema mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara ameshambuliwa kwa kupigwa na watu wasiofahamika.
Post a Comment
Powered by Blogger.