LIVERPOOL YAICHAKAZA BARCELONA KWA MAGOLI MANNE BILA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Timu ya Liverpool ya Uingereza imeichakaza Barcelona kwa magoli 4-0 katika mchezo wa kombe la Kimataifa la Mabigwa katika dimba la Wembley.

Katika mchezo huo Sadio Mane alikuwa wakwanza kuifungia Liverpool goli kufuatia shambulizi lililofanywa kwa kuwahusisha Adam Lallana na Philippe Coutinho.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Javier Mascherano alijifunga baada ya kipindi cha pili na kuizawadia timu yake hiyo ya zamani goli la pili.

Divock Origi aliongeza goli la tatu kwa Liverpool kwa kuupitisha mpira kati kati ya miguu ya Claudio Bravo na baadaye Marko Grujic alifunga goli la nne kwa kichwa cha kunyanyua.
             Mchezaji mpya wa Liverpool Sadio Mane akiifungia timu hiyo goli la kwanza
          Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi akishangilia goli lake alilofunga 
        Kipigo kikiwaacha hoi wachezaji wa Barcelona Luis Suarez na Lionel Messi
Post a Comment
Powered by Blogger.