LEO KATIKA HISTORIA: SOMA HAPA WASIFU WA HAYATI ABOUD JUMBE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Aboud Jumbe alizaliwa Juni 14, 1920 Mkamasini, Unguja. Alishika madaraka ya kuiongoza Zanzibar mwaka 1972 baada ya kifo cha Mzee Abeid Amani Karume, kilichotokana kwa kupigwa risasi siku ya Ijumaa jioni Aprili 7, 1972 Makao Makuu ya Afro Shirazi Party (sasa ofisi kuu ya CCM) Kisiwandui, Zanzibar.

Akiwa na Shahada ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Mzee Jumbe anatajwa kuwa muasisi wa mageuzi ya demokrasia Zanzibar, aliyefungua milango na kutoa nafasi kubwa kwa wananchi, kushiriki na kutoa maoni yao katika ujenzi wa nchi.

Baada ya mapinduzi ya Januari 12, 1964 Zanzibar haikuwa na Katiba, hivyo maamuzi ya nchi yalikuwa yakifanywa na Baraza la Mapinduzi kwa niaba ya wananchi. Alhaji Jumbe ndiye aliyeanzisha mchakato wa matayarisho ya kuundwa kwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 mchakato ulioanza mwaka 1979, ukijumuisha mambo ya msingi kama haki za binadamu, utawala bora na uhuru wa kutoa maoni.

Ni Katiba hiyo ndio Januari 13, 1980 iliunda Baraza la Wawakilishi na kuwa chombo muhimu cha kusikiliza na kuwasilisha maoni ya wananchi. Likitenganishwa kikazi na Baraza la Mapinduzi.

Akizindua Baraza la kwanza la Wawakilishi, Alhaji Jumbe alisema: “Hiki chombo ni ngomeya wananchi…kitakuwa muhimu katika kuwakilisha maoni ya wananchi katika ujenzi wa demokrasia na utawala bora,”.

Pamoja na Baraza hilo, Katiba hiyo iliimarisha mhimili mwingine wa dola wa Mahakama, kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki zao za msingi, bila kuingiliwa na yeyote.

Alhaji Jumbe, aliwaleta Zanzibar wanasheria kadhaa wakiwamo Bashir Swanzy kutoka Ghana na Damian Lubuva kutoka Bara (Tanganyika)

Aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakar alimtaja Mzee Jumbe kama kiongozi aliyefanya kazi kubwa kuimarisha demokrasia iliyokuwa imefungiwa milango kwa muda mrefu.

“Kwa kuanzisha Baraza la Wawakilishi…kuimarisha Mahakama na kada ya wanasheria kunaweza kumpa Alhaji Jumbe sifa ya kuwa Baba wa demokrasia Zanzibar.,” anasema Bakari.

Abubakar Khamis Bakari, alikuwa Katibu wa kwanza wa Baraza la Wawakilishi na kwa nyakati tofauti alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar.

Ni Mzee Jumbe ndiye aliweka mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu ya Dola, Zanzibar.

Baraza la Wawakilishi, Mahakama na Serikali iliyokuwa chini ya Rais na Waziri Kiongozi aliyewajibika kumsaidia rais na kiongozi wa shughuli za kila siku za Baraza la Wawakilishi na utendaji wa Serikali.

Mafanikio ya kazi zake

Miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo matunda yake yanaonekana hadi leo, ni kuzaliwa kwa CCM Februari 5, 1977 kwenye uwanja wa Amani, mjini Unguja.

Ule ulikuwa uamuzi wa kishujaa sana, ni kitendo ambacho watu wengi hawakukitarajia, kuvizika vyama maarufu vilivyoshiriki mapambano ya kudai uhuru na Mapinduzi, si jambo dogo.

Kazi kubwa iliyofanywa na Tanu (Tanganyika)yaani kudai uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Mwingereza.

Inafahamika kama inavyofahamika na kuenziwa kwa kazi ya Afro Shirazi Party (ASP) chini ya Mzee Karume ya Mapinduzi ya mwaka1964 na kumaliza

Usultani wa Mwarabu wa Oman.
Kauli inayokumbukwa na wananchi wa Zanzibar ya kuiaga ASP, iliyotamkwa na vijanawa halaiki ni:

“Afro mama tunakuaga …si kama umetufanyia baya…lakini

Muungano kwetu niusawa Afro!”

Sherehe hizo zilihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi, na CCM ikazaliwa na kuongozwa na Mwalimu Julius Nyerere akiwaMwenyekiti wa kwanza wa CCM huku Alhaji Aboud Jumbe, akiwa Makamu wake.

Kama Mzee Jumbe, asingekubali rai ya kuunganisha vyama, pengine leo tusingekuwa na CCM.

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Makame Mzee anasema Aboud Jumbe, alikuwa na majukumu mazito ya kutekeleza dhana ya Mapinduzi na ilani ya ASP, ambayo ni maisha bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuandaa makazi bora ya nyumba za kisasa.

“Baada ya kifo cha Sheikh Karume…Sheikh Jumbe ndiye alionekana kuwa mrithi wake sahihi kwenye Urais…Na kweli – alitekeleza kwa kiasi kikubwa Ilani ya ASP,” anasema Makame Mzee.
Post a Comment
Powered by Blogger.