LEO KATIKA HISTORIA: MTAMBUE MOHAMMED IQBAL DAR MBUNIFU WA JINA LA "TANZANIA"

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


"MOHAMMED IQBAL DAR" Huyu ndiye aliebuni neno "Tanzania" Muhammed Iqbal Dar ni nani? 
Ni mtoto wa dkt Tufail Ahmad Dar, alizaliwa mkoani Tanga mwaka 1944 baba yake alikuwa daktari mwenye asili ya kihindi huko mkoani Morogoro. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya H H D AGHAKHAN baadae akajiunga Mzumbe akasoma kidato cha 1 hadi cha 6.

Ilipofika mwaka 1964 baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar muungano wa nchi hizi mbili ulizalisha jina la "Republic of Tanganyika & Zanzibar" jina hili lilionekana kuwa ni lefu sana ndipo serikali ikaandaa shindano la kutunga jina fupi na zuri litakalojumuisha nchi zote 2 yani Tanganyika na Zanzibar, Tangazo la shindano lilitolewa ktk gazeti la "Tanganyika Standard" ambalo hv sasa linaitwa daily news.

Muhammad Iqbal baada ya kupata tangazo hili ndipo akaanza halakati za kushiriki ktk shindano, anasimulia mwenyewe kuwa alichukua karatasi na akaanza kuandika "Bismillah Rahman Rahiim" kisha akaandika jina la TANGANYIKA alafu akaandika ZANZIBAR kisha akaandika jina lake la ubini ambalo ni IQBAL kisha akaandika jina la jumuiya yake ambayo ni AHMADIYA, baada ya hapo akamuuomba mwenyemungu amsaidie kupata jina zuri kutoka katika majina hayo aloyaandika hapo juu, baada ya hapo alichukua herufi tatu za mwanzo kutoka ktk neno Tanganyika yani "TAN" then akachukua herufi tatu za mwanzo kutoka ktk neno Zanzibar yani ZAN alivyounganisha TAN+ZAN akapata TANZAN alafu akachukua elufi ya kwanza ktk jina lake Iqbal ambayo ni "I" alafu akachukua elufi ya kwanza kutoka ktk jumuiya yake ya Ahmadiya ambayo ni "A" hapa jina la Tanzania ndipo likapatikana TAN+ZAN+I+A kwa mantiki hii Tanzania imepatikana kutoka ktk majina manne ambayo ni Tanganyika+Zanzibar+Iqbal+Ahmadiya.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo Muhammad akalituma jina hlo ktk kamati ya kuratibu shindano, baada ya muda mwingi kupita baba yake Muhammad Iqbal mzee Tufail Ahmad Dar alipokea barua mzito kutoka serikalini ikimfahamisha kuwa mwanawe ndo ameibuka mshindi ktk shindano hlo.
Post a Comment
Powered by Blogger.