MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » » GAZETI LA MSETO LAFUNGIWA MIEZI 36


Pamoja Blog 8/11/2016 07:00:00 PM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kulifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 leo Agosti 11, 2016 katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

Na Shamimu Nyaki WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amelifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 kutokana na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.

Uamuzi huo wa kulifungia gazeti la Mseto umetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 242 lilitolewa tarehe 10Agosti 2016 kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 Sura ya 229, Kifungu 25(1).

Mhe. Nape Moses Nnauye ameeleza kuwa Kifungu hicho kinampa mamlaka yeye kama Waziri kuchukua uamuzi wa kufungia Gazeti kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.

“Serikali kwa masikitiko makubwa imelazimika kilifungia gazeti la Mseto kutokana na mwenendo wa uandishi wa kuandika na kuchapisha habari za uongo na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali kwa nia ya kumchafua Rais wetu wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt.John Pombe Mgufuli na viongozi wa Serikali” Alisema Mhe Waziri Nape.

Aidha Mhe. Nape amesema kuwa hatua ya kulifungia gazeti la Mseto imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Septemba,2012 hadi Agosti,2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kuacha kuandika habari za upotoshaji,uchochezi na za uongo na zisizo zingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa Habari bila mafanikio.

Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayoanisha Uhuru wa Habari na mipaka ya habari kama vile tamko la Haki za Binaadamu la mwaka 1948 ambapo nchi yetu imeruhusu kwa kiwango kikubwa kwa kuweka ukomo wa uhuru huo kwa kukataza habari za uzushi uongo na uchochezi.

Gazeti la Mseto limezuiwa kuchapishwa katika njia nyingine yeyote ikiwemo mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.


CHANZO: MICHUZI BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments