ALIKIBA, LADY JAY DEE KUKIWASHA TAMASHA LA SEREBUKA KESHO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wasanii Alikiba, lady jay dee na wengine wengi kesho kushusha burudani ya Nguvu katika viwanja vya posta ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili ambapo tamasha hilo likiwa na lengo la kuwashukuru watanzania kwa kutoa sapoti kubwa sana katika kuangalia Chaneli hiyo inayopatikana katika Vig'amuzi vya Startimes pekee. Tamasha la Serebuka limedhaminiwa na HUAWEI Tanzania
Tamasha hilo litapambwa pia na Wasanii mbalimbali kutoka bongo movie huku wasanii kama Eskide mkali wa singeli atashusha burudani ambayo kila atakayehudhuria atafurahishwa nayo. 
Tamasha la Serebuka Litaanza saa nne asubuhi katika viwanja vya Posta Kijitonyama huku baadhi ya Huduma na bidhaa za startimes zitapatikana pia kama vile TV, Simu, Projector pamoja na Dekoda za Startimes.
Kiingilio cha Tamasha hilo ni Shilingi Elfu Tano tu. Karibu wote
Post a Comment
Powered by Blogger.