UTAFITI: UNYONYAJI WA VIDOLE UNA FAIDA KWA WATOTO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni na jarida la utafiti wa kisayansi la Pediatrics limesema kuwa watoto wanaonyonya vidole au kung’ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.


Theluthi moja ya watoto hao ni wanyonyaji wa vidole mara kwa mara au hung’ata kucha zao na katika vipimo walivyofanyiwa watoto hao wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

Watoto wengi wameonekana kuathirika kutokana na mazingira ya hali ya hewa pamoja na kula vyakula fulani, lakini unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana kuzuia baadhi ya allergy na matatizo hayo.

Kati ya watu elfu moja wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 32 walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand. Aidha jarida hilo limesema kuwa tabia hiyo ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.
Post a Comment
Powered by Blogger.