URENO YA MUONGEZEA MKATABA KOCHA FERNANDO SANTOS HADI 2020

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kocha wa Ureno, Fernando Santos ameongezewa mkataba hadi 2020 na chama cha soka cha Ureno-FPF baada ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kutwaa taji la michuano ya Ulaya mwaka huu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho toka Septemba mwaka 2014, aliiongoza Ureno kutwaa taji lake la kwanza kubwa la kimataifa pamoja na kucheza bila nyota wake Cristiano Ronaldo katika fainali dhidi ya wenyeji Ufaransa mapema mwezi huu.

Mkataba wake mpya alioongezwa utamfanya kukiongoza kikosi hicho katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na ile ya ijayo ya Ulaya. Santos amewahi kufundisha klabu kubwa nchini Ureno zikiwemo Benfica, Sporting Lisbon na Porto huku pia akiwahi kuinoa timu ya taifa ya Ugiriki.
Post a Comment
Powered by Blogger.