UPDATES: BASI LA UDA LAGONGA TRENI ENEO LA GEREZANI – KARIAKOO JIJINI DAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ajali imetokea usiku huu kati ya treni na basi la Uda linalofanya safari zake kati ya Kariakoo na Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.
“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana na hivi ninavyozungumza na wewe naelekea Muhimbili,” amesema Kaimu kamanda huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.