TRA YAGAWA MASHINE ZA EFD KWA WIZARA ZINAZOKUSANYA MADUHULI YA SERIKALI.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akimkabadhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya mashine tano kwaajili ya wizara yake ili kila wanapofanya malipo mbalimbali mapato ya TRA yakatwe.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akionyesha Mashine za Kiletroniki za EFDs ya mfano kabla ya kugawa kwa mashine tano katika wizara zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, ambazo zitakuwa kwaajili ya kukusanya mapato katika wizara hizo.
 Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akitoa maelekezo ya Mashine za Kieletroniki mbele ya makatibu wa kuu wa wizara pamoja na wawakilishi wa wizara mablimbali jijini Dar es Salaam leo kabla ya Kuanza kugawa katika wizara zote za serikali. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) imegawa Mashine za Kieletroniki za EFDs tano kwa kila katibu Mkuu wa Wizara kwa ajili ya kukusanya maduhuli ya serikali kwa kutumia mashine hizo.

 Hatua hiyo imetokana na agizo la  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wizara zinazotoa huduma ziwe na mashine za EFD ili kuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa taifa.

 Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa ugawaji wa mashine hizo kwa taasisi za serikali zitasaidia kutunza  kumbukumbu katika kupanga maduhuli.

“Mashine hizi ni lengo serikali katika kuhakikisha wananchi wanaopata huduma wanapata risiti kwa kutambua umuhimu wa kodi kwa huduma wanazopata”amesema Kidata.

Aidha amesema mashine hizo ni mashine za kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa za kisasa katika kutunza kumbukumbu za huduma ambazo wanazitoa.

Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah Mwandumbya amesema kuwa watawafundisha wakuu wa idara hizo jinsi ya kuzitumia.
Imeandaliwa na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii.
Post a Comment
Powered by Blogger.