TGNP YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUJADILI MKATABA WA MAENDELEO YA KIJINSI WA SADC

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu akizungumza jambo kwa wanachama wa mtandao wa Itifaki ya kijinsi waliokutana kupitia mkataba wa nyongeza wa Maendeleo na jinsia wa SADC.

Mwezeshaji kutoka Sung Consultancy Firm Bw. Husein Sengu akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka asasi binafsi na za kiserikali katika ukumbi wa Seashells Jijini Dar.
MTANDAO wa jinsia nchini (TGNP) kwa kushirikiana na Asasi wanachama wa mtandao wa Itifaki ya kijinsi wamekutana kupitia mkataba wa nyongeza wa Maendeleo na jinsia wa SADC wa mwaka 2015
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano huo ulioshirikisha asasi na wadau mbalimbali pamoja na wawakirishi kutoka serikalini, Meneja wa Ujenzi wa nguvu ya pamoja wa TGNP, Grace Kisetu alisema warsha hiyo inalenga kutoa makubaliano ya mkataba huo.
Alisema kupitia mkataba huo wa hiari ambao unatarajiwa kusainiwa na marais wa nchi wanachama wa SADC August mwaka huu utaondoa baadhi ya sheria ambazo zinaonekana kukinzana.
“Ukiangalia sheria ya ndoa za utotoni ya SADC ya mwaka 2008 inakinzana na sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 2001 ambapo ya SADC inasema kuwa mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 aruhusiwi kuoa au kuolewa wakati ya hapa inasema mtoto wa umri wa miaka 14 anaweza kuolewa kwa ridha ya wazazi au mahakama.
“Lakini mkataba huu,kuhusu sheria hiyo imezuia kabisa na imeweka wazi kwamba hakutakuwa na ndoa yoyote kwa mtu mwenye urmi chini ya miaka 18 jambo ambalo linaendena na tafsiri yetu ya mtoto.
“Pia kwenye mkataba umetamka wazi kwamba sheria zote hata zakwenye katiba ziweze kutenguliwa na kupitia sheria kandamizi na zile zinazohusu ukatili wa kijinsia kuzitunga mpya ili kuendana na sheria hii ya Kimataifa na ya Kikanda,” alisema Grace.


Pia aliishauri Serikali kuangalia namna ya kuipitia na kuifanyia marekebisho sheria ya kimila ambayo imekuwa ikikandamiza haki ya mjane.
Baadhi ya wadau kutoka asasi mbalimbali wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa  kuhusu mkataba huo wa hiari ambao unatarajiwa kusainiwa na marais wa nchi wanachama wa SADC 

Baadhi ya wadau kutoka asasi mbalimbali wakichangia mada


Picha ya pamoja

Post a Comment
Powered by Blogger.