PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA MIA MOJA AROBAINI(140)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Kabla ya safari Shamim aliwasiliana na Hussein na kumuomba waongozane katika safari hiyo kwa sababu ya kuweka uwezekano wa tatizo kutokea basi ingebidi Hussein aingilie kati na kusaidia. "Hussein hakuna anayekufahamu hapa Tanzania kwa sababu hiyo nachukua tahadhali mapema! Tusijekujikuta tunapata matatizo na kukamatwa wote na akakosa wa kumsaidia mwenzake! Hivyo wakati tunatoka naomba ubaki nyuma na mwanangu Alex jr"akasema Shamim. "Ok bosi nimekwelewa!"akasema Hussein.
"Mumy! Kuna tatizo?"akauliza mtoto Alex. "Nothing my son! Kila kitu kiko sawa kabisa"akajibu Shamim Mtoto alivyoongea hivyo kuna kitu kilitokea ghafla kwenye moyo wa Shamim na akahisi kuumia sana moyo. Ilibidi ainame chini na kutulia kwa muda akijiuliza kilichotokea ninini? Moja kwa moja akachukulia hiyo kama ishara ya huko mbele lazima kuna tatizo litatokea na mambo hayatakuwa mepesi.
Ile hali ilidumu kwa dakika kama tano kisha ikaisha. Junior yeye hakuwa na wasiwasi wala hakutaka kujishughulisha na chochote juu ya wale. Muda huo yeye alikuwa kaweka earphone zake masikioni akisikiliza mziki wa Maria Carey. Wakati wao wanakuja na ndege huku Tanzania timu ya wanajeshi waliofuzu katika mafunzo yote ya kikomandoo walishawasili uwanja wa ndege na kuchukua nafasi zao wakisubiria mtu wao awasili.
Wote walikuwa wamevaa nguo za kawaida sana lakini wakiwa wamejizatiti vya kutosha ili kupambana na Shamim. Mawaziri wale wawili,mkuu wa majeshi na kijana Martin wote pia walikuwa pale pale uwanjani sehemu ya kupokelea abiria wakisubiri muda utimie wafanye kazi.

Shamim ndege waliyopanda ilipitia Cairo kisha ikasimama pia Nairobi. Shamim aliwashauri wenzie washukie pale na kutafuta namna ya kuingia Tanzania bila kupitia uwanja wa ndege ila Junior alikuwa king'ang'anizi akidai amechoka sana hivyo hakutaka usumbufu.
Aliwalazimisha mpaka wakakubaliana naye na uzuri Junior na Shamim walikuwa wamebadilisha sura na kuwekewa sura za bandia hicho kilimpa kujiamini ila hakujua kuwa picha ya sura ya bandia ya Shamim ilishafikia idara zote za polisi. Walifika uwanja wa ndege kama muda uliopangwa ikiwa ni saa tisa zajioni.
Waliposhuka walipita eneo la ukaguzi bila shida huku Shamim akitembeza macho yake kwa kasi kuangalia kama kuna wana usalama pale. Mpaka wanaingia eneo la mapokezi hakuona sura ya kuitilia wasiwasi ila alipotokeza tu sura yake eneo la mapokezi aliona sura kadhaa ambazo alihisi moja kwa moja kuwa ni askari kutokana na uzoefu wake kwa hawa viumbe.
"Hussein rudi nyuma kabisa tuwe mbali kuna tatizo"aliongea kwa kutumia vyombo vyake vya mawasiliano na kumfikia Hussein aliyemchukua mtoto na kujifanya kuzunguka zunguka kwa nyuma zaidi. "Tunaomba usimame hivo ulivyo na uko chini ya ulinzi! Ukileta ubishi wowote ule umekwisha"aliambiwa na mmoja wa maafisa aliowaona pale. Wale mawaziri na mkuu wa jeshi wakiwa na Martini walinyenyuka na kusogea eneo lile.
Walipofika walikuta Shamim akiwa anawaangalia wale maafisa wa jeshi akijiuliza cha kufanya pale. Junior alipaniki na kuhalibu picha nzima. "Nyie mna akili? Mnanifaham?"aliongea kwa kujiamini kwa sababu alijua ana sura badia. Kosa lingine likafatia kutoka kwa Junior na ambalo wale viongozi wakubwa walitaka litokee ili wapate cha kujitetea kuwa walikuwa wakipambana. Junior akasogea na kumshika Shamim ili waondoke.
Bastora tano zilitoka kwenye viuno vya wale viongozi watano na kuwalekea akina Shamim. Kwa sababu alikuwa mwepesi akashtukia lile tendo na kumshika Junior akamgeuzia upande wa pili ili wakwepe zile risasi. Viongozi wale hawakufanya makosa wakaachia risasi kadhaa kuelekea walipokuwa akina Junior. Ingawa Shamim alijalibu kukwepa ila wingi wa zile risasi na eneo kuwa dogo vikamponza na risasi kadhaa zikapenya kwenye mwili wake. Viongozi wale hawakuacha kupiga risasi.
Shamim aliendelea kunyeshewa mvua ya risasi sehemu mbali mbali za mwili wake wakati Junior alishaaga Dunia kitambo. Walipohakikisha hatikisiki wakaita waandishi waliowaanda na kuongea nao. "Mara nyingi sana jeshi la polisi limeshindwa kumdhibiti huyu gaidi wa kike ila leo tumeamua kuingilia kati na tumefanikiwa kummaliza"waliongea kifupi na kuahidi wakutane ukumbi wa habari kwa maelezo zaidi.
Wakati tendo lile linatokea Alex jr aliona na kushtuka ila Huusein akamziba mdomo na kugeukia kwingine. Alex jr aliwaona wale viongozi watano wakati wakimalizia kumuua mama yake pale chini na kuwakalili. Kesho yake vyombo vya habari vyote vikatawala swala la kuuawa kwa Shamim huku wale viongozi watano wakijichukulia sifa kubwa na wengine kupandiswha vyeo.
Shamim alizikwa na serikali kwa siri bila mtu yeyote kufahamu alikozikwa na wala kuhudhulia mazishi. Hussein aliondoka na yule mtoto Alex jr kurudi Marekani na kuishi naye. Habari ya Shamim serikali ikajua imeizikia hapo!! Haikujua!! Haikujua!! Haikujua Shamim alikuwa na mtoto na kawaida mtoto wa nyoka ni nyoka!!

..........................................................................
MWISHO

SASA JIANDAE NA HADITHI MPYA YA "NAJUTA KUMSALITI MPENZI WANGU "

Post a Comment
Powered by Blogger.