PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA MIA MOJA THELASINI NA SABA (137)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu."Nimemaliza kazi ya kwanza ya kumteketeza Abdul napaswa nihakikishe mzigo wangu naupata kisha nipumzike haya mambo ya mapambano kwa ajili ya mwanangu aliyeko tumboni"alisema Shamim. "Sawa bosi ila kumbuka Junior katoloka na askari wanakutafuta! Tunakwepa vip hilo?"akauliza Hussein. "Junior hajatoloka ila aliyetoloka ni Kisu! Alipomfikisha pale Bagamoyo alirudi kumkomboa na nilishajua hilo tangu mwanzo hivyo niliandaa vijana wangu wakapambana nao na kuwashinda! 
Ila Kisu aliweza kufanikiwa kumtoa GPS Junior ila hakufanikiwa kuondoka naye"akasema Shamim. "Kwa sasa Junior yuko wap? Na Kisu tunamfanyaje?"akauliza Hussein.
"Hussein leo nilipokuwa napambana nimeshindwa kwa sababu ya hiki kiumbe! Nahitaj kuachana na haya mambo ya mapambano ili nisijempoteza mwanangu! So andaa safari tuondoke kuelekea Mexico"akasema Shamim Kwa sababu kikwazo kikubwa kwake kilikuwa ni Abdul hivyo haikumuwia vigumu kuanza mipango ya safari mara baada ya kubadilisha sura yake na kutumia miongoni mwa sura kadhaa bandia alizokuwa nazo.
Hussein aliandaa taratibu za safari ile mpaka ilipokamilika. 
Wakati huo huo Shamim alijalibu kila njia kumshawishi Junior asahau kuhusu Joan na waanze maisha upya huku wakijiandaa kulea mtoto wao. Kwa Junior ilikuwa ngumu ila alikubali ili aondoke kwenye mabalaa ya hapa nchini lakini akipanga huko mbele atawageuka wenzake na kutokomea. Safari ilipokamilika walikwea pipa na kuelekea Mexico kwa amani bila bughudha.

Walipokelewa uwanja wa ndege na matajiri wa kiMexico waliokuwa wakishilikiana na Shamim katika biashara. Shamim alipotoka gerezani aliwasiliana na hawa matajiri nao wakawatafuta wale vijana wake waliomsaliti na kuwakamata kabla hawajauza mzigo ule. Hivyo siku hiyo Shamim alipelekwa mpaka sehemu waliyofungiwa na kuwaona. "Hawa sitawaua ila naomba wasipewe chakula mpaka siku wakifa kwa njaa"alisema Shamim.
Matajiri wale waliokuwa wakiufaham uwezo wa Shamim na wakimuogopa sana walitii na kutelekeza kila alichoagiza. Shamim alipewa pesa kutokana na mauzo ya ule mzigo na kisha yeye akamgawia Hussein asilimia thelathini ya kile kilichopatikana. "Nakutakia maisha mema Hussein popote utakapopenda kuishi na ukiwa na shida wasiliana nami kupitia zile njia zetu za mawasiliano"alisema Shamim. Walikumbatiana huku kila mmoja akitoa machozi na kisha Hussein akaondoka.
Shamim aliondoka na Junior na kwenda kuishi Marekani kwenye mji wa Maryland na wakanunua eneo kubwa kwenye ufukwe wa Beach Heaven na kujenga mjengo wa maana kisha wakaishi kwa amani. Upendo na amani ilianza kutawala kwenye maisha ya Shamim na Junior na taratibu Junior akaanza kumsahau Joan na kuanza kumpenda Shamim hasa kutokana na Kiumbe alichokuwa nacho.
Miezi saba mbele Shamim alijifungua mtoto kwenye Hospital ya Asbury Hospital. Walifanikiwa kupata mtoto wa kiume waliyempatia jina la Alex kama ukumbusho wa kaka yake Junior. Miaka mitatu baadae. Mpelelezi maarufu nchini Tanzania aliyefatilia kwa muda mrefu juu ya taarifa za gaidi wa Kisomali kama wao walivyoamini alipata mgeni ofisini kwake.
"Naitwa Kisu"alijitambulisha. "Kisu!? Jitambulishe kwa jina lako halisi kijana hapa ni sehemu ya usalama wa Taifa sio unakuja na majina ya ajabu ajabu hapa"akafoka Martin. "Naitwa Jacob Sulleiman maarufu kama Kisu"akajibu. "Hilo ndo jina sasa4 enhee!! Unashida gani kijana?"akauliza Martin. "Nina taarifa muhimu sana za kuweza kukusaidia wewe"akaongea kwa kituo Kisu. Martin alitulia na kumwangalia kwa makini Kisu.
"Taarifa za kunisaidia mimi! Enheee! Taarifa gani hizo?"akauliza Martin. "Ni kuhusu gaidi ambaye amekuwa akiisumbua akili yako kwa zaidi ya miaka mitatu Shamim"akasema kwa kituo Kisu. Martin alishtuka na kusimama wima!! Akamtazama vizuri kisu.

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.