PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA MIA MOJA ISHIRINI NA SABA(127)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Vijana wale waliendelea kubishana juu ya lile swala la ule mzigo wa Shamim kama wanapaswa kuuza kisha wagawane pesa au waende kumkomboa kisha wauze naye na yeye ndiye awape mgao wao. "Mimi nashangaa mnachobishana hapa! Kwani huu mzigo ni wa kwake? Si kawazurumu Wasomali wake? Sasa sisi tukimdhulumu inakuwaje shida? Acheni ushamba huu ni wakati wa kupiga pesa"akasema mmoja wa wale waliokuwa wakitaka wauchukue.
"Nawaambia ukweli kuuchukua huu mzigo ni kujiweka kwenye wakati mgumu sana kwa sababu hata Abdul na yeye anautaka kwa sababu yeye ndiye kiongozi wa kikosi kwa sasa! Jaman acheni roho ya hivyo"akajibu mmoja. Waliendelea kulumbana kwa muda na wale waliotaka wauchukue na kuuza wakamshawishi mmoja wa wale waliokuwa wanapinga mpaka na yeye akakubali. Akabaki mmoja aliyefahamika kwa jina la Hussein, yeye alikataa katakata kumsaliti Shamim hata kwa upinde kwa sababu aliufahamu uwezo wake. Wakati anaendelea kuwalazimisha wenzie wamwelewe walipeana ishara kisha wakanyenyuka na kuanza kupambana naye.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.