PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA MIA MOJA ISHIRINI NA SITA(126)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Shamim alikuwa mpole lakini kichwani akiwa na hasira kali sana huku pia akipanga namna ya kuwatoka wale askari. Alipelekwa mpaka chini kutoka ndani ya gari ile. "Piga magoti chini binti"aliamrishwa.
Shamim hakuwa na cha kubisha bali alinyenyekea. Askari mmoja alikabidhi silaha kwa wenzie na kumfata Shamim pale chini akamkunja mikono kwa nyuma kisha akamfunga pingu. Shamim alishindwa kumtumia yule askari kutoloka kutokana na kutokuja na silaha ambayo ingemsaidia Shamim katika kutoloka na pili wingi wa wale askari ulimtisha.
Junior aliitwa eneo lile na wale askari. "Kijana umesema huyu binti ni nani?"akauliza aliyeonekana kuwa kamanda wa kile kikosi. "Huyu ni yule mwanamke gaidi aliyewahi kufanya tukio la kuwaua askari Mwenge miaka miwili iliyopita na akapotea"akajibu huku akiwa anaogopa sana. "Kijana una uhakika? Kumbuka yule ni gaidi ambaye askari kibao walishindwa kumdhibiti sasa mbona kawa mpole sana hapa? Au umemfananisha?"akauliza tena yule askari.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.