PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA MIA MOJA ISHIRINI NA MBILI(122)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Gari iliondolewa kwa kasi ya ajabu kutoka eneo lile na kuacha vumbi likitimka. Alex hakuwa nyuma bali na yeye akiwa na vijana wake waliondoa gari lao kasi kumfatilia Shamim na watu wake. Uwezo wa gari waliyokuwa wakiitumia akina Shamim na ile Noah waliyokuwa nayo akina Alex vilikuwa vitu tofauti. Hivyo walipotoka kwenye barabara za vumbi na kuingia kwenye lami Shamim waliwaacha akina Alex mbali sana. Na walipowaacha Shamim akacheza mchezo.
Akachukua simu yake na kupiga namba ya Alex. "Uko wap mme wangu?"alianza na swali mara baada ya simu kupokelewa. "Niko njiani kuna sehemu naenda mamaa"akajibu Alex bila kufahamu kuwa anayemfukuzia ndiye anayeongea naye. "Naomba nije kwako babaa"akasema Shamim. Lile swali lilikuwa gumu kwa Alex kujibu!
"Baba niko njiani nakuja kwako basi nijibu"akasema Shamim. "Niko mbali kidogo mke"akajibu Alex. "Mimi sitaki hayo maelezo bali nataka uje sasa hivi! Kwani mimi na hayo unayofanya kipi cha muhimu?"akauliza kimtego Shamim. "Basi mama nakuja sasa hivi"akajibu Alex.UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWAITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.