MWILI WA JOSEPH SANGA WAWASILI LEO JIJINI DAR, KUAGWA KESHO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa baada ya kuwasili kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 kutoka nchini India. 
Marehemu Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Waombolezaji wakiweka jeneza lililobeba mwili wa  marehemu Joseph Senga kwenye gari  kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili
Simanzi ikiwa imetawala mara baaya kuwasili kwa mwili wa Marehemu Sanga
Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo
Baadhi ya Waandishi wa habari waliofika kuupokea mwili wa marehemu Sanga aliyefariki nchini India
Marehemu Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima likitoka uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na kuelekea katika Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa kwa mwili huo.
Post a Comment
Powered by Blogger.