MSIBA WA MPIGAPICHA JOSEPH SENGA WAWAKUTANISHA LOWASSA, MBOWE NA NAPE, WANAHABARI WAFURIKA, MAJONZI YATAWALA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MWILI wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, linalomilikiwa na kampuni ya Free Medea, Joseph Senga, umeagwa jijini Dar es Salaam leo Julai 31, 2016 na tayari umesafirishwa kwenda wilayani Kwimba mmoani Mwanza alikozaliwa tayari kwa mazishi. Katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu, Mamia ya Waandishi wa Habari, Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali, wananchi na wanasiasa walifurika kwenye ibada hiyo na jambo kubwa zaidi, msiba huo umewakutanisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Marehemu Senga alifariki nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo na mwili wake tayari uko njiani kuelekea wilayani Kwimba kwa amzishi.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, ndiye aliyeongoza mamia ya waombolezaji kutoa heshima za mwisho, na kufuatiwa na Waziri Nape , Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na Katibu Muu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa E;lisante Ole Gabriel. Pichani juu, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, akisalimiana na Waziri Nape Nnauye.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, (kulia), akizungumza na Waziri Nape Nnauye(kushoto)
Ni majonzi na vilio


Mbowe akitoa hotuba yake kwa niaba ya kampuni ya Free Medea na CHADEMA
Mke wa Marehemu Joseph Senga, akisadiwa wakati akiwasili kwenye eneo la ibada
Mke wa Marehemu akiwa na mwanae
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, (kulia), akilakiwa na Mwandishi wa Habari Mkongwe ambaye kwa sasa ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi
Waziri Nape akitoa salamu za serikali
Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni ya The Guardian Limited, Selemani Mpochi, akitoa salamu za chama cha Wapiga Picha Tanzania.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA), Innocent Mungi, kwa niaba ya Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali akitoa salamu za kwa niaba ya wenzake
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, akitoa salamu za wana Ubungo, ambako marehemu alikuwa kiishi kwenye jimbo hilo
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akizunguzma
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Senga
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, akitoa heshima zake

Meneja Uhusiano wa Vodacom, Matina Nkurulu, akitoa heshima zake mbele ya marehemu Senga
Wakazi wa Sinza na maeneo mengine ya jiji wakitoa hshima zao
Mungi akitia heshima zake
Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Manyerere Jacton, (mwenye koti jeusi) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (ECF), Sebera Fulgence(mwenye t-shirt), na waombolezaji wengine wakitoa heshima zao
Meneja Uhusiano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafuzni wa Elimu ya Juu, Omoga Ngole ( mwenye t-shirt) nyeusi), pamoja na waombolezaji wengine wakitoa heshima zao
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na waandishiw a habari wakitoa hesima zao
Makamu mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, (mwenye nguo nyeusi) na baadhi ya waandishi wa habari na wananchi wengine wakitoa heshima zao

Waandishi wakongwe, Jacklin Liana, (kushoto), akifurahia jambo na Angetile Osiah
Jeneza la marehemu likipelekwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Kwimba mkoani Mwanza
Post a Comment
Powered by Blogger.