MJI WA MEDINA WASHAMBULIWA NA MAGAIDI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua katikati ya Jiji la Media jirani na Msikiti wa Mtume. Jiji la Medina ni miongoni mwa miji mitakatifu kwa mujibu wa Imani za Kiislamu.
Kituo cha Televisheni cha Arabiya kimesema mlipuaji huyo alitekeleza unyama huo wakati maofisa wa usalama wakifuturu.
Habari kutoka mjini humo zimesema maofisa wawili wameuawa, lakini hakuna taarifa rasmi ya kiserikali iliyotolewa hadi sasa. Msikiti wa Mtume ndipo alipozikwa Mtu SAW na jiji hilo ni mji mtakatifu wa pili kwa Waislamu nyuma ua Mecca.
Mapema iliripotiwa kuwapo kwa taarifa za kushambuliwa kwa roketi mji Qatif unaokaliwa na Waislamu wengi wa dhehebu la Shia, na mshambuliaji aliulenga msikiti, lakini hakufanikiwa kuuharibu.
Post a Comment
Powered by Blogger.