LINAH ADAI BADO ANA NAFASI YAKUFANYA MAKUBWA KWENYE MUZIKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii wa muziki wa kike aliyewai kufanya vizuri na wimbo ‘Oletemba’ Linah Sanga amefunguka kwa kusema kuwa
kwa sasa yupo chimbo kuandaa kazi yake mpya audio pamoja na video ambazo amedai zinakuja kuruidisha heshima yake katika soko la muziki wa bongofleva.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa hana management ameiambia Bongo5 kuwa bila hata uongozi yeye mwenyewe naweza kufanya kazi kubwa ambayo itawashangaza mashabiiki wake wa muziki.
“Mimi najiamini sana, mimi ni msanii ambaye siwezi kukata tamaa katika maisha yangu ya muziki, mimi ni jeshi la mtu mmoja,” alisema Linah “Nafasi ya kufanya vizuri kwenye muziki ninayo tena bila hata wasiwasi, na kwa sasa anajipanga kivingine kabisa, kwa hiyo naweza sema mashabiki wa muziki wangu wasubirie audio a video soon,”
Aliongeza, “Mimi ni msanii mkubwa na tayari nimeshafanya mambo makubwa katika huu muziki bado na hit nyingi, kwa hiyo nafasi au kitu kama hicho ni CV katika muziki wangu, yaani naweza kusema tayari na mtaji wa fans base ya kutosha ambayo inaweza kuusapoti muziki wangu,”
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Imani’ ambao aliutoa miezi michache iliyopita.
Post a Comment
Powered by Blogger.