FEDERER KUKOSA OLIMPIKI 2016 KUFUATIA MAUMIVU YA GOTI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mchezaji wa tennis Mswisi, Roger Federer ametangaza hatoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu.
Ametoa tangazo lake hilo kufuatia maumivu ya goti aliyoyapata na kufanyiwa upasuaji mwezi Februari hali iliyomsababisha kuzikosa French Open zilizofanyika mwezi Mei.

Mapumziko haya ya Federer yatamfanya kuikosa michezo yote ya msimu wa mwaka huu. Amesema anahitaji kujijenga upya iwapo anataka kuendelea na mchezo wake wa tennis.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema anasikitika kwa kutoiwakilisha nchi yake ya Uswisi huko Brazil katika mashindano ya Olimpiki na anajisikia vibaya kupoteza muda wa msimu uliosalia.

Source: BBC
Post a Comment
Powered by Blogger.