UPENDO WOMEN’S GROUP YA UBELGIJI YAFANYA HARAMBEE YA KUISADIA HOSPITALI YA MWANANYAMALA TANZANIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mgeni rasmi Dr.Guido Nicolai akifungua hotuba maalumu kuhusu Harambee ya kuchangia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.Kikundi cha Upendo Womens Group kilichopo nchini Ubelgiji jana tarehe 11.06.2016 walifanya Arambee hiyo kuwasaidia kina mama wanaojifungua katika mazingira magumu nchini Tanzania 
Kiongozi mkuu wa kikundi cha kina mama wa Upendo Group Mh; Theresia Greca, muda mfupi kabla ya ufunguzi wa shughuli za uchangishaji wa fedha ili kusaidia kina mama wanaojifungua katika mazingiza magumu katika hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Viongozi na wananchama wa Upendo Women’s Group wakipata picha ya pamoja 
Mweka hazina wa kikundi cha Upendo women’s Group Begum Chunny akitoa maelewo mafupi jinsi alivyoenda Tanzania kukagua maendeleo yao yanayopatkana katika kuchangia hospital ya Mwananyamala,kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Mrs Theresia Greca.
Wageni mbalimbali walihudhuria shughuli hiyo 
Wageni mbalimbali walihudhuria shughuli hiyo 
Kina mama wa Upendo wakiingia ukumbini kwa shangwe huku wakiimba nyimbo ya kuisifia Tanzania 
Burudani ya muziki wa Jazz ilitumbuizwa na kikundi cha JAIL CITY VETERAN,watu waliburudika sana na muziki huo 
Mitindo na tamaduni mbalimbali za kitanzania zilionyeshwa ukumbini hapo,pichani bidada Chantal katikati akiwa na wasichana wadogo wa kitanzania wakiwaonyesha wageni waliohudhuria maisha ya kitanzania 
Bidada Jacky akionyesha wazungu jinsi ya kukuna nazi kwa kibao cha mbuzi,huu ndio utamaduni halisi wa mtanzania 
Vazi la khanga kwa wasichana warembo lilishika chati ukumbini hapo 

Ubunifu wa mavazi ya asili ya kitanzania kwa mavazi ya baharini,angalia jinsi hawa wawili walivyopedeza.Kumbuka hii ni katika shughuli ya uchangishaji wa kuisadia hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,Na kazi yote hii ni jitihada za kikundi cha Upendo Women’s Group cha Ubelgiji. 
Mwanadada Chantal akionyesha vazi la Kimasai katika maonyesho ya mavazi ili kuchangia fedha katika hospital ya Mwananyamala..Dada huyu kajitolea dola za kimarekani 500 
Utamaduni wa mwambao wa pwani pia ulionyeshwa, hapo kina kaka na madada kwa mbali wakionyesha utamaduni wa mzanzibari 
Mmoja wa wawakilishi wa Lions Club Wetteren Rozenstreek ya Ubelgiji akikabidhi hundi kwa wana Upendo Women’s Group 
Mwakilishi wa Inne wheel wetteren akimkabidhi hundi mwenyekiti wa Upendo Women’s Group Mrs Theresia Greca katika kuchangia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania 
Wana Upendo Group baada ya shughuli za uchangishaji kuendelea pia walitoa sadaka ya chakula kwa kila mgeni aliyefika ukumbini hapo 
Wageni wakiendelea kupata chakula.
(Picha zote na Maganga One Blog)
Post a Comment
Powered by Blogger.