UPDATES: WAPINZANI WABEBA MABANGO, WATOKA BUNGENI MBELE YA WAGENI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Wabunge wa upinzani wakitoka bungeni muda mfupi kabla ya Bajeti ya Serikali kuanza kusomwa.
Wabunge wa upinzani wametoka tena bungeni, safari hii wakiwa wameshika mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti kuonyesha kutoridhishwa kwao na uongozi wa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Wabunge hao wamefanya hivyo mbele ya wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi walioalikwa kusikiliza hotuba ya bajeti inayowasilishwa hivi sasa na Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango.
Leo imekuwa siku ya tisa wabunge wao wakitoka bungeni kusisitiza ujumbe wao huo huku wakiwa tayari wameandika barua ya kutaka Dk Tulia aondolewe kwa azimio la kutokuwa na imani naye.
Post a Comment
Powered by Blogger.