TUNDU LISSU NA MHARIRI WA MAWIO WAFIKISHWA KIZIMBANI LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wakili wa upande wa utetezi alikuwa ni Wakili Msomi Peter Kibatala na washitakiwa waliofika ni namba 2 na 3 ambao ni Bwana Ismair na Mkina washtakiwa wengine akiwepo Tundu Antiphas Lissu hawakuhudhuria mahakamani kwa sababu mbalimbali.

Mashitaka walisomewa ni matano na washitakiwa wote ndugu Mkina na Ismair walikataaa mashitaka yote matano. Pia kwasababu washitakiwa wengine hawapo akiwepo Tundu Antiphas Lissu, mahakama iliombwa itoe wito kwa washitakiwa kufika mahakamani.

Peter Kibatala akisaidiwa na mawakili wawili anawaombea washitakiwa walioko mahakamani mdhamana kwa masharti nafuu. Kwasababu wametii na kujisalimisha mahakamani wenyewe. Dhamana ilikuwa wazi kwa washitakiwa hao wawili, na kila mmoja anatakiwa kudhaminiwa na watu wawili watakaoweka saini ya Bond

Washitakiwa woote walipewa dhamana na kesi itatajwa tena tarehe 28/06/2016
Post a Comment
Powered by Blogger.