PROFESA LIPUMBA AOMBA KURUDI CUF NA KUPEWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesitisha mpango wake wa kung’atuka kwenye wadhfa huo baada ya kushawishiwa na viongozi wa dini, chama hicho na wanachama.
Profesa Lipumba aliyetangaza kuachana na uongozi wa chama hicho, Agosti 8 mwaka jana baada ya CUF kukubaliana na Ukawa kumsimamisha Edward Lowassa kuwania urais, ameomba kwa barua kurejea kwenye wadhifa wake, ambao umekuwa unashikiliwa kwa muda na mwanasheria, Twaha Tasilima.
Katika barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad juu, Lipumba amesema, “Nimekuja kuongeza nguvu baada ya hitilafu za uchaguzi mkuu wa Zanzibar, harakati za kuipata demokrasia zinahitaji umoja wa wote wenye nia moja.”
Post a Comment
Powered by Blogger.