PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA MIA MOJA NA TISA(109)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Maandalizi ya Shamim kurudi Tanzania kwa ajili ya kukutana na Alex ili kuhakikisha anapata uwezekano wa kujua ulipo mzigo wa bosi wake. Siku mbili baadae safari iliwadia na Shamim akakwea ndege na kuelekea Tanzania akiwaacha Abdul na Majid wakiwa na Bosi wao wakielekea Mombasa kwa ajili ya kusubiria majibu ya kazi aliyotumwa. Alifika Tanzania na cha kushangaza Alex hakuja kumpokea uwanja wa ndege bali vijana wale sita waliopangwa na bosi wake kufanya naye kazi kwa Tanzania ndiyo waliokuwa pale uwanjani kumpokea.
"Nipe ripoti ya Alex"akauliza. "Amendoka saa mbili asubuhi na Emirates Airways kuelekea Dubai na anatarajiwa kurudi baada ya siku mbili kulingana na tiketi zake"akajibiwa. "Nipe ripoti ya Joan mdogo wangu"akauliza tena. "Amehamishiwa Kisumu na anamalizia kidato cha tatu ila afya yake ilileta mgogoro siku chache zilizopita na akapata matibabu kwa sasa yuko sawa kabisa"akajibiwa.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA 

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.