MCHEZAJI WA ZAMANI WA NIGERIA NA KOCHA STEPHEN KESHI AMEFARIKI DUNIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mchezaji wa zamani wa Nigeria na baadaye akaja kuwa kocha wa Timu hiyo ya Super Eagles Stephen Okechukwu Chinedu Keshi ameiaga Dunia saa chache zilizopita.
Emmanuel Ado, kaka wa marehemu amesema Keshi amefariki mapema leo Jumatano, Juni 8. “Kwa mapenzi yake Mungu, familia ya Ogbuenyi Fredrick Keshi inatangaza kifo cha Mr. Stephen Okechukwu Chinedu Keshi,” ilisema taarifa hiyo ya Ado.

Taarifa hiyo ikaendelea: “Mtoto wetu, kaka yetu, baba yetu, mkwe wetu, shemeji yetu, amekwenda kuungana na mkewe (Nkemu) Bi Kate Keshi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 35 Disemba 9, 2015.

“Tangu mkewe alipofariki, Keshi alikuwa kwenye maombolezo. Alirejea Nigeria kuwa naye. Alipanga kuondoka leo kurejea Ulaya, kabla hajapata matatizo ya moyo na kufariki.


“Mke wa Keshi alifariki kwa ugonjwa wa kansa.

Watu wake wa karibu wanasema hakuwa na tatizo lolote la afya lakini inadhaniwa amepatwa mshituko wa moyo.

Keshi aliyewahi kutwaa tuzo ya kocha bora Afrika, aliwahi pia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo.
Post a Comment
Powered by Blogger.